Raia wa Catalonia leo hii watachagua viongozi wao wapya, katika uchaguzi ambao serikali kuu ya Uhispania inaamini utamaliza msuguano wa kisiasa unaoendelea.
Serikali kuu ya Madrid iliuvunja utawala uliokuwepo awali, baada ya kuandaa kura ya maoni iliyotajwa kuwa haikufuata kanuni, iliyotaka uhuru wa eneo hilo.
Rais wa Catalonia aliyeondolewa madarakani, Carles Puigdemont, amekuwa akiendeleza kampeni zake za kujitenga na Madrid akiwa uhamishoni chini Ubelgiji kwa kupitia mitandao ya kijamii.
Mwezi Oktoba yalifanyika maandamano makubwa ya Catalonia kutaka kujitenga na Hispania
Mwezi Oktoba yalifanyika maandamano makubwa ya Catalonia kutaka kujitenga na Hispania
Takwimu zinaonyesha kuwa vyama vinavyotaka kujitenga na vile vinavyotaka kusalia kwenye serikali ya Madrid vinalingana katika kura za maoni.
Kuna kila dalili uchaguzi huu ukaibua tena hisia za kutaka kujitenga kuliko kutatua matatizo.