Chadema Waijia Juu CCM "Hatutaki Yajirudie ya Idi Amin"

Chadema Yaijia Juu CCM "Hatutaki Yajirudie ya Idi Amin"
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekosoa kitendo cha CCM kuweka mgombea wake kwenye nafasi ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki wakati haikutakiwa kufanywa hivyo, na kusema kwamba kitendo hicho kitasababisha mgogoro wa kidiplomasia.


Kwenye taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kutoka kwa chama hiko, imesema CCM imekiuka utaratibu wa Bunge hilo la kumtafuta Spika la kuliongoza kwa kumuweka mtu wao kwenye kinyang'anyiro, wakati kiutaratibu ilitakiwa Spika wa awamu hii atoke nchi ya Rwanda kulingana na mzunguko ambao ulikuwa unafuatwa, na kwamba kitendo hicho kinaweza kuleta migogoro itakayoathiri Jumuiya hiyo kama kipindi cha Idi Amin.

"Awamu hii Spika alipaswa kutoka Rwanda, lakini Tanzania kwa kuwa CCM imezoea kutokuheshimu sheria na kanuni zilizopo imemteua mbunge wake Adam Kimbisa kugombea nafasi ya Spika kinyume kabisa na kanuni za Bunge hilo, na huu ukiwa ni mwendelezo wa utamaduni wao wa kutokuheshimu sheria na kanuni, kitendo ambacho kinatishia ustawi na uwepo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki", imeandika Taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa .."CHADEMA tunalaani kitendo hiki, CCM wajue kuwa watabeba lawama zote kama kutakuwa na mgogoro ndani ya Bunge la Afrika Mashariki ambayo unaweza kupelekea mgogoro wa kidiplomasia katika Jumuiya nzima kutokana na tabia yao ya kutoheshimu taratibu zilizowekwa. Ttunataka kanuni za EAC ziheshimiwe, kwani tunakumbuka matendo ya Idd Amin mwaka 1977 yalivyovunja

 Jumuiya hii, hatutaki yajirudie kamwe".
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa huu ni ugonjwa wa akili au ndio laana ya kukosa uzalendo wa nchi inawaandama Chadema? Sasa Chadema wamekuwa wasemaji wa Rwanda? Vipi mtu au taasisi yenye utimamu wa ufahamu ifananishe masuala ya kidoplomasia na uvamizi wa nchi ya jarani yake uliofanywa na Iddi Amin?
    Je kama uspika huo wa bunge la Africa mashariki unatija kwa Tanzania kinachowaasha Chadema ni kitu gani? Kwanini Chadema watangulize uchama kwanza kuliko uatifa katika masuala ya kigeni? Je kama huyo kada wa CCM anaediwa na Chadema kupendekezwa na serikali ya cha mapinduzi kushika nyazifa hiyo ya uspika ubunge wa Africa mashariki akipita na kuchaguliwa kushika wazifa huo atakuwa spika wa bunge anaeotoka CCM au anaetokea Tanzania? Wakati mwengine watanzania tusidanganyike kuwa hivi nyama ya siasa aina yakina Chadema vipo kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu hapana ni usaliti mtupu uliovigubika hivi vyama kwa nchi yetu na ni wakati kwa watanzania kuachana na ushabiki wa kijinga au sijui ukanda kuvisapoti hivi vyama tutangulize maslahi ya Taifa kwanza.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad