Chama cha ANC Chaanza Kumsaka Mrithi wa Zuma

Chama cha ANC Chaanza Kumsaka Mrithi wa Zuma
Chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC kimeanza mkutano wa siku tano kumchagua kiongozi mpya.

Kuna mchuano mkali wa pande mbili unaoonekana wakati huu muhimu katika historia ya Taifa hilo baada ya ubaguzi wa rangi.

Mshindi atakayepatikana katika mkutano ulioanza leo Jumamosi Desemba 16,2017 ataandaliwa kuwa Rais ajaye wa Afrika Kusini.

Chama cha ANC kimepoteza umaarufu kwa kiasi kikubwa tangu Nelson Mandela alipokiweka madarakani katika uchaguzi wa mwaka 1994 ambao uliweka ukomo wa utawala wa Wazungu wachache.

Rais Jacob Zuma ambaye utawala wake umekumbwa na kashfa za rushwa atang'atuka madarakani kama kiongozi mkuu wa ANC lakini atasalia kuwa mkuu wa nchi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2019.

Wanaowania uongozi wa chama ni mke wa zamani wa Rais Zuma na aliyekuwa mkuu wa Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma na Naibu Rais, Cyril Ramaphosa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad