Diva Afunguka Mapenzi Yalivyomponza Msanii Heri Muziki Hadi Kusababisha Kufeli Masomo

Diva Afunguka Mapenzi Yalivyomponza Msanii Heri Muziki Hadi Kusababisha Kufeli Masomo
Kumekuwa na tetesi kuwa mapenzi yanamfanya msanii wa Bongo Fleva, Heri Muziki kufanya vibaya kwenye masomo yake ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM). Sahau kuhusu hizo tetesi kwani tayari wote wawili yaani Heri Muziki na mchumba wake ‘Diva The Bawse’ wamezungumzia ukweli uliopo.

Heri Muziki amekataa kuwa kufeli kwake masomo kunatokana na mahusiano ya kimapenzi na mtangazaji wa Clouds FM, Diva The Bawse, kwa kusema kuwa kufeli kwa mwanafunzi yeyote ni jambo la kawaida na sio kitu cha kushangaa huku akikataa kuwa kufanya kwake vibaya kwenye masomo hakujasababishwa na mapenzi kama watu wengi wanavyodai.

“Unajua kupata sapu chuo ni kitu cha kawaida lakini hiyo stori ya sapu (Supplementary) nyingi ndio naisikia hapa leo but thats not a case siwezi nikasema thats a case… Nilikuwa nafanya muziki nipo shule na ikaongezeka pia na mahisiano vitu ambavyo kila kitu kilikuwa kinahitaji muda… And it was my first time kuwa kwenye mahusiano na mtu maarufu iliniyumbisha kidogo  kwa muda mfupi lakini nikarudi kwenye hali yangu baada ya kuzoea, lakini sio chanzo (cha kufeli).“amesema Heri Muziki kwenye kipindi cha Playlist cha Times FM.

Hata hivyo Bongo5 imemtafuta Diva kuzungumzia ishu hiyo ambapo Diva amekiri kuzisikia taarifa hizo na kusema kuwa yeye sio chanzo kwani huwa anamsaidia kwenye masomo yake kwa hali na mali.

Diva amesema kuwa huwa anamsapoti Heri Muziki kwani anajua umuhimu wa elimu katika maisha na anatamani siku moja mchumba wake nae apate cheti kama yeye.

“I have been very supportive about Heri na elimu yake. When it comes to me nimeenda shule na nimefika level ya Chuo pia so naelewa umuhimu wa elimu katika maisha . If you love someone huwezi muacha aharibikiwe katika shule au kazi anayofanya, utajitahid kumuelewesha hapa na pale na maamuzi huwa ni yake mwisho wa siku.”amesema Diva na kuzungumzia jinsi anavyosapoti muziki wake.

“Sihusiki na Heri kutoa au kutotoa muziki wake kwani ana management yake they know better, all in all i always try to tell him kipi kizuri na kibaya ila he has his own decisions to make in life. Na kingine I’m a fan of his work ni shabiki wake mkubwa sana hivyo would love to see him anafika kilele cha mafanikio. Im very proud of him, He is a smart, loving, caring and one of a kind human being. Hivyo i always wish him well regardless.“amesema Diva.

Heri Muziki jana ameachia ngoma yake mpya inayoitwa ‘Roho Juu’ akiwa ameshirikiana na Otuck William itazame hapa chini kisha dondosha maoni yako.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad