Dk. Tulia Ataka Mambo ya Siasa Zitengwe

Dk. Tulia Ataka Mambo ya Siasa Zitengwe

Naibu Spika Dk. Tulia Ackson amefanya ziara katika baadhi ya maeneo wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya kutekeleza baadhi ya ahadi alizotoa na kusema kwamba lazima mambo ya maendeleo yatengwe mbali na siasa kwani rais wa nchi anapiga marufuku tendo hilo.


Dk Tulia amesema hayo wakati akitoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni tano katika shule ya sekondari Bujela

"Niwasihi jambo moja ambalo hata Rais Magufuli husisitiza, tusiingize siasa kwenye mambo ya maendeleo kwasababu  bila hivyo hatutapiga hatua, leo kama TULIA TRUST tuliahidi vifaa vyenye thamani ya Milioni tano na tayari tumetekeleza kwa kuja navyo vikiwemo bati, mbao, mchanga, saruji, chokaa, rangi, vioo, nondo," amesema Dk. Tulia

“Tunafanya haya yote kwa ajili ya kuhakikisha tunawatengenezea watoto wetu mazingira mazuri ya kujisomea na baadae watuletee maendeleo sisi wazazi wao hivyo niwaombe viongozi wote tushikamane,” Dk Tulia.

Pamoja na hayo Dk. Tulia alifika katika kanisa la Bujela ambalo liliharibiwa kwa upepo uliosababishwa na mvua na kuchangia jumla ya mabati 100 yenye thamani zaidi ya milioni mbili Kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa kanisa hilo ambalo tayari ujenzi wake ulianza kwa jitihada za waumini wenyewe.

Dk. Tulia amewahimiza waumini pamoja na viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa la Tanzania amani pamoja na kumuombea Rais Magufuli ili aendelee kuiongoza nchi salama.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa maendeleo hayana chama hila chama ndio kina maendeleo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad