Dr. Shika amesema wakati Babu Seya anaingia nchini Tanzania yeye alikuwa nje ya nchi hivyo hajawahi kumuona lakini anafahamu nyimbo zake ambazo aliwahi kuimba.
''Simfahamu Babu Seya, wakati anaingia nchini tayari nilishaondoka nchini muda mrefu, lakini nafahamu nyimbo zake ile aliyoimba baba na mwana tunaimba na kucheza ndio haswa naifahamu vizuri'', amesema.
Pia Dr. Shika amempongeza Rais Magufuli kwa kuwatoa wafungwa mbali mbalimbali na kutumia vizuri fursa ya uongozi kama mkuu wa nchi. ''Nampongeza Rais Magufuli kwa tukio hili la kuwatoa wafungwa na kuwapa uhuru wakaanze maisha yao upya'', ameongeza.
Nguza Viking maarufu kama ''Babu Seya'' na Johnson Nguza ''Papii Kocha'' walipatikana na hatia ya kubaka na kunajisi watoto na walihukumiwa kwenda jela maisha tangu mwaka 2004 kabla ya kupata msamaha mwaka huu wakiwa wamedumu gerezani kwa miaka 13.