Mtanzania Dkt. Louis Shika aliyejizolea umaarufu mkubwa hivi karibuni katika mitandao na vyombo vya habari ameeleza sababu ya kuacha kufanya matangazo ya kibiashara na kampuni mbali mbali.
Umaarufu wa Dkt. Shika ulikuja baada ya kujitokeza katika mnada wa kuuza nyumba za Lugumi ambapo aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800, kisha kudai anangojea fedha zake kutoka nchini Urusi.
Dkt. Shika amekiambia kipindi cha Weekend Breakfast cha EA Radio kuwa ameacha kufanya matangazo kwa kuhofiwa kufuatiliwa na maadui zake kutoka nchi ya Urusi alipokuwa akifanya kazi miaka ya nyuma.
“Sina interest na haya matangazo tena kwa sababu wale Warusi niliowakimbia watani-track watajua niko wapi, lakini natoa ushirikiano kwa wenzangu huku nikiwa nimetafuta means nyingine za kuwakwepa,” amesema Dkt. Shika.
Dkt. Shika ameweza kufanya tangazo la kampuni moja ya michezo ya ubashiri matokeo katika soka, pia ameweza kuonekana katika video mbili za nyimbo za Bongo Flava. Video hizo ni za Kundi la Rostam ‘Kiba_100’ na wimbo wa Gaza ‘Nanii’ akishirikiana na Madee.
Tena kuwa mwangalifu na lazima uwe na mabodi gari.
ReplyDeleteAngalia meneja Wako asikuuze na kuchukua chake. Umesha walipa Wabongo??
Kwani ugomvi na hao najambazi waliokuteka wakitaka uwape pesa bado unandelea? Bado wanataka uwape pesa? Majambazi huwa wana-target mtu kwa kipindi cha miaka mingi hivyo? Yule mmoja si alishauwawa? Na wale wengine Kwani polisi urusi ilishindwa kuwakamata? Km polisi ilifanikiwa kuwasaka, naamimi wameshahukumiwa, hivyo, nguvu yao ya kukufuatilia pengine imepungua au haipo. Halafu, kukufuatilia ni gharama na sifikiri km watakuwa radhi kuendelea na business ambayo ulipofanikiwa kuwtoroka, kwao Hiyo ilikuwa ni hasara,haikulipa.after all, kulingana na maelezo yako inaonyesha walikuwa ni watu wa kujidunga sindano za kulevya. Watumiaji wa ulevi huo huwa hawana uwezo wa kufocus jambo kwa mud a mrefu, Kwani uwezo wao wa kumbukumbu hasa za short term ninakuwa zimeathirika na madawa ya kujidunga. Zaidi ya yote muda tayari umepita km walikuwa vijana, basi sasa ni watu wazima. Usiogope Dr, ila unaweza kuogopa tu iwapo sabbabu ulizotuelezea kuhusiana na kutekwa kwako zilikuwa manufactured
ReplyDeleteShika luisi shika Visa unayo?
ReplyDelete