Trump:Amechukua maamuzi yaliyowashinda marais waliopita wa marekani.
Mwaka 1995 bunge la marekani lilipitisha Sheria ya kuhamishia ubalozi wa USA katika mji wa Jerusalemu.
Trump ameitambua jerusalem kama mji mkuu wa israel na kuamuru mchakato wa kujenga ubalozi uanze mara moja.
Netanyahu:Amemshukuru Rais Trump kwa uamuzi wake na amesema hakutakuwa na amani ya kweli bila Jerusalemu kutambulika kama ni makao makuu ya israel bila kugawanywa.
Hata hivyo Israel itaheshimu umuhimu wa kiimani katika Jerusalem.ameomba mataifa mengine kama UK na German kuungana na US kuitambua Jerusalem kama makao makuu ya israel.
UNSG GUTERES:Hakuna njia bora na mbadala wa amani zaidi ya two state solution.
Suala la Jerusalemu ni la mwisho na muhimu katika majadiliano.
Ameonya juu ya Taifa moja kufanya maamuzi bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa.
Hamas:Tangazo la Trump limefungua milango ya kuzimu kwa maslahi ya marekani mashariki ya kati.