Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza kupanda bei ya mafuta ya taa, petroli na dizeli kulinganisha na Novemba Mosi, 2017.
Bei za rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa Sh41 kwa lita sawa na asilimia 1.96; Sh30 (asilimia 1.54) na Sh3 (asilimia 0.17) kwa mfuatano huo.
Bei ya jumla ya petroli, dizeli na mafuta ya taa imeongezeka kwa Sh41.42 sawa na asilimia 2.06, Sh30 (asilimia 1.63) na Sh3.27 (asilimia 0.18) kwa mfuatano huo.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godwin Samwel, ongezeko la bei kuanzia leo Jumatano Desemba 6,2017 limetokana na ongezeko la gharama za usafirishaji.
Amesema licha ya kuimarika kwa shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani fedha inayotumika kununulia mafuta, kumekuwa na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo.