Muigizaji wa filamu nchini, Faiza Ally amesema baada ya kuposti picha akiwa leba mtandaoni watu wengi wamemkosoa lakini sio kwa watu wote walioona ile picha ni mbaya kwani Marafiki zake, mumewe na familia yake wamechukulia tukio hilo kwa furaha na kumpongeza .
Faiza Ally amesema sio watu wote walichukizwa na picha ile kwani baadhi ya watu walimpongeza kwa kuona amezaa bila kufanyiwa upasuaji kitu ambacho wanawake wengi wa siku hizi wanaogopa.
Kwa upande mwingine Faiza amesema amewasamehe watanzania kwa kuwa kwa wengi wao ni kitu kigeni lakini kwake ni jambo la kawaida kutokana na maisha yake aliyoyapitia akiwa nje ya nchi.
Faiza Afunguka Kuhusu Kupost Picha Akwa Leba Anajifungua "Nimepongezwa na Wengi"
3
December 06, 2017
Tags
Kweli mtoto anachukua akili ya mzazi
ReplyDeleteHuyu Malaya ana matatizo ya akili. Jambo jengine na la kusikitisha kabisa inaonekana serikali kupitia mamlaka husika imeshindwa kabisa kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao Tanzania. Halafu utasikia kuna malalamiko ya mmong'gonyoko wa maadili? Vipi unakwenda kulalamika kwa jirani kwamba unakosa amani mvua inaponyesha kutokana ubovu wa paa la nyumba yako wakati suluhisho rahisi ni kuziba tu ile sehemu inayovuja kwenye paa au ikiwezekana hata kuenzua paa lote na kulisuka upya. Watu wengi wana mikanda yao mbali mbali ya filamu juu ya mambo yao binafsi lakini sio haki hata kidogo kuweka kila uchafu wa mtu kwenye mitandao ya kijamii. Ndipo ninapojiuliza serikali iko wapi? Vyombo vinavyohusika na matumizi mabaya ya mitandao viko viko? Hakuna kitu rahisi na cha haraka kuenea katika jamii yeyote hivi sasa kama mawasilianao yanayopatikana kwa njia ya utandawazi kupitia simu nakadhalika. Kuanzia mtoto wa miaka mitano 5 kwendea juu wana uwezo wa kufikia mawasilianao ya internet na kuangalia nini kinachoendelea ndani yake. Najiulia Tanzania inaelekea kujenga taifa la kizazi cha kesho cha namna gani? Mtu kufanya mambo ya hovyo kwa kisingizio ati aliishi nje ya nchi ni sababu za kiulimbukeni. Nimekuwa ninaishi nje karibu maisha yangu yote kama ilivyo kwa baadhi ya Watanzania kadhaa wanaoishi huku nje maeneo mbali mbali duniani lakini watakubalina nami yakwamba tumekuwa nikishuhudia mambo mengi sana ya aibu yakisambazwa Tanzania katika mitandao ya kijamii kinyume na tamaduni zetu za kiafrika na kidini . Hapa hatuzungumzii demokrasi au uhuru wa vyombo vya habari. Tunazungumzia maadili na taratibu za nchi. Kwa Mfano mimi kama muafrika na kutokana na imani yangu ya dini naruhusika kuoa wake wawili au hata watatu kunako makubaliyano maalum na wanawake husika ambao tutakuwa tunaishi katika misingi ya ndoa na nafikiri sitakua na kesi yeyote ya kujibu kwenye serikali ya Tanzania juu ya ndoa yangu ya ukewenza lakini ndoa hiyo hiyo nikiifunga hapa Marekanni ni kifungo cha miaka mingi tu na kama nina watoto wanataifishwa wanakuwa si wangu tena. Kwa mfano katika mitandao ya kijamii ya Tanzania unaweza kuona wanasambaza picha mbali mbali za matukio kama mtu aliekufa bila kuziba sura yake. Au kama ajali imetokea basi utaona picha mbali mbali za majeruhi zikiwa wazi kabisa zikionesha hali mbaya za majeruhi lakini vitu kama hivyo huwezi kuona vikichapishwa hovyo katika mitandao ya kijamii ya Marekani wanaadabu licha yakuwa nchi yenye kuheshimu uhuru watu kupitiliza kiasi lakini jambo lakujifunza ni kwamba kila nchi inataratibu zake na kama unataka kuishi pale lazima uzifuate au utalazimishwa kuzifuata kabla hujaleta karaha kwa watu wengine.
ReplyDeleteNenda zako punguani we! Hao waliokupongeza punguani kama wewe, nyote hamna maadili wala dini. Kwani kuzaa tunu? hata mbwa na paka wanazaa. Ovyooooooooooooooooooooooooooooooo
ReplyDelete