Nape kupitia mtandao wake wa Instgram jana aliandika "Ni rahisi kuchukulia poa kwasababu kwako mambo yanaenda, lakini sio hata kidogo" jambo ambalo liliwafanya wananchi waanze kueleza hisia

Wiki kadhaa zilizopita Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa anachukizwa sana na kitendo cha watu kutafsiri kauli zake anazozitoa kwenye mitandao ya kijamii na kuzihusisha na kumsema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Maguifuli.
