Haya Ndio Maneno Aliyoandika Zahir Zorro “Nikifa Nitalala kwa Amani”

Haya Ndio Maneno Aliyoandika Zahir Zorro “Nikifa Nitalala kwa Amani”
Mwanamuziki mkongwe nchini  Zahir Zorro ambaye aliingia kwenye tasnia ya muziki 1968 na alifahamika zaidi alipokuwa kwenye band ya JKT Kimulimuli ambapo aliendelea kutamba kwenye fani hiyo sambamba na watoto wake Banana na Maunda Zorro.

Zahir Zorro amechukua headlines kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuandika historia fupi ya maisha yake pamoja na watoto wake Maunda na Banana, alitamani sana kuishi Ulaya akiwa bado mwenye umri mdogo kwani alijua hela inapatikana nje ya Afrika.



Mama yake Zahir Zorro hakutaka mwanae atoke nje ya Afrika na kusema kuwa elfu 75 ni bei ya gari aina ya Peugeot 504 na kuwa sio hela kubwa ya kumudu maisha nje ya Afrika na ana uwezo wa kumnunulia gari hilo, hivyo ajiunge na jeshi kwanza.

Gari aina ya Peugeot 504



Ila kwa upande wa baba yake Zahir Zorro alitamani sana mwanae apitie maisha ya jeshi ili siku moja akifariki akapumzike kwa Amani akijua kuwa ameacha mtu imara mwenye uwezo wa kuisimamia familia yao, na hivyo alijiunga na kulitumikia jeshi kwa miaka 16.

Zahir Zorro hakuweza kufata mila na destruri za kijeshi na hakutaka watoto wake wapitie huko hivyo ilimgharimu kuwatafutia mwalimu wa Martial Arts(mafunzo ya karate) na mwisho wake Maunda alijiunga na Jeshi la Polisi lakini mwisho wa siku hakuweza kulitumikia jeshi hilo.



Baada ya yote hayo Banana Zorro alipata nafasi na bahati ya kuishi Uingereza lakini baada ya kuishi huko wiki mbili  alitamani apate uraia ili aishi huko milele ila kuna msemo unasema nyumbani ni nyumbani na hivyo Banana alirudi nyumbani kutokana na kumkumbuka sana baba yake “Nimekukumbuka sana siwezi kuishi mbali na wewe”



Zahir Zorro alitamba na ngoma zake tofauti tofauti zikiwemo Beatrice, Cleopatra, Danga Che na Chiku lala salama.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad