Madereva katika kituo cha mabasi cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam wamelalamikia upatikanaji wa abiria kuwa mdogo katika kipindi hiki cha sikuu, kutokana na watu wengi kutokuwepo mjini.
Madereva hao sambamba na makondakta wametoa kilio chao hicho wakati huu baada ya abiria wengi kusafiri kwenda mikoani kuungana na familia zao kwa ajili ya sikukuu za Krismasi na mwaka mpya, na neema kuwaangukia wenzao wanaoendesha mabasi ya mikoani.
Wakizungumza na waandishi wa habari madereva hao wamesema ukosefu wa abiria kumewaathiri kipato chao cha kila siku, hali inayopelekea mabosi zao kutowaamini kwa kuwa wamezoea kufanya ruti kumi kwa siku na kipato kuwa cha juu, lakini kwa sasa wanafanya ruti tatu hadi tano kwa siku, hali inayochangia kushuka kwa makusanyo ya mapato yao ya kila siku.