Idadi Kubwa ya Views YouTube ni Kipimo cha Wimbo Kukubalika?, Nikki wa Pili Afunguka

Rapper wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amejibu iwapo idadi kubwa ya views YouTube inayopata wimbo inaweza kutumika kama kigezo cha wimbo husika kukubalika.

Nikki wa Pili amesema ni sawa kwa asilimia kati ya 50 au 60 lakini cha muhimu ni wasanii kujijengea ushawishi katika mitandao ili kuwa na idadi kubwa ya wanaofuatilia kazi zao.

“Hapo kuna vitu viwili kwa msanii ambaye tayari ana ushawishi mkubwa kwenye media anapotoa wimbo watu wanakuja kuangalia, lakini pia unapotoa wimbo maadui zako na watu wanaokupenda wanakuja kukuangalia aidha wimbo ni mzuri au mbaya” Nikki ameiambia Bongo5.

“Lakini hata wale watu ambao hawakupendi wanaweza kuja kuangalia, kwa hivyo views za YouTube zina nafasi kwa asilimia 50/60 zinaonyesha huo wimbo umekubalika. Kwa hiyo nafikiri ni wasanii kujenga ushawishi kwenye social media ili anapotoa kazi yake kuwe na watu wengi wanaenda kuuangalia” amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad