IGP Sirro: Malalamiko Yatolewayo na Viongozi wa Upinzani dhidi ya Polisi Katika Uchaguzi Mdogo si ya Kweli

Mkuu wa jeshi la polisi nchini(IGP) Simoni Sirro, amesema tuhuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuwa polisi walihusika kuwatoa nje wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika hivi karibuni si za kweli kwa sababu hajawahi kupokea barua ama malalamiko ndani ya ofisi yake kutoka kwa viongozi hao.

IGP Sirro ameyasema hayo mkoani Lindi, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kwamba tuhuma hizo zinazotolewa na viongozi hao si za kweli kwani hajawai kupata malalamiko hayo na kusema kuwa kama kuna mtu ana ushahidi na tukio hilo atoe taarifa mara moja ndani ya jeshi la polisi ili waweze kupeleleza na kuchukua hatua.

Chanzo; ITV
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad