Jacqueline Wolper, Leo Kusheherekea Sherehe Yake ya Kuzaliwa

Jacqueline Wolper, Leo Kusheherekea Sherehe Yake ya Kuzaliwa
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper, leo anatarajia kufanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa huko Masaki katika ukumbi wa Buckets ambapo atazindua ‘Application’ ambayo itapatikana kwenye Google Play Store ya duka lake la nguo kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa ukaribu.

Msanii atakayepiga shoo katika hafla hiyo ni Barnaba Classic  kuanzia saa moja mpaka saa sita usiku.  Wolper amemchagua Barnaba kupiga shoo hiyo kwa kuwa ni msanii anayempenda na kumsapoti kwa ukaribu akisema nyimbo zote alizoimba zinaelezea maisha yake aliyoyapitia.
Staahuyo amewaomba mashabiki zake kufika kwa wingi katika ukumbi wa Buckets kumsapoti na amesema kiingilio ni shilingi 10,000/- tu.
Wasanii mbalimbali wengine  watakuwepo kumsapoti Wolper leo.  Pia amesema shangwe za siku yake ya kuzaliwa zitaendelea kesho mjini Dodoma katika klabu ya usiku ya burudani ya Maisha.  Amewaomba pia mashabiki zake wa mji huo kujitokeza kwa wingi kumsapoti.
Kampuni ya Global Group tunamtakia Wolper kila la heri katika siku yake ya kuzaliwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad