Akizungumza na wana habari leo, Kamanda wa Kanda Maalum hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa awali jambazi huyo alimkodi dereva pikipiki ili ampeleke maeneo ya msitu huko Buza.
Kamanda Mambosasa amesema kuwa ghafla walipofika eneo hilo jambazi huyo alitoa bastola yake iliyotengenezwa kienyeji ikiwa na baruti na kumuamuru dereva ashuke na kumuachia pikipiki. Baada ya kushuka dereva alipiga kelele kuomba msaada na ndipo wananchi walijitokeza na kuanza kumpiga kwa mawe huku wengine wakimkata mapanga jambazi huyo.
Alieleza kuwa askari walipopata taarifa walipofika eneo hilo walimkuta jambazi huyo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na ndipo walimkimbiza katika hospitali ya Temeke kwa ajili ya matibabu na muda mfupi baadae alifariki dunia.
Hata hivyo marehemu huyo anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (25-30) na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Temeke kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitaalamu.