Je, Jacob Zuma Kuondolewa Madarakani Kama Rais wa Afrika Kusini?

Je, Jacob Zuma Kuondolewa Madarakani Kama Rais wa Afrika Kusini?
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma inawezekana asimalize muhula wake wa mwisho madarakani baada ya chama cha ANC kumchagua Cyril Ramaphosa kama kiongozi wake mkuu.

Kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, Ramaphosa alikua rafiki wa karibu wa Zuma na hata msaidizi wake, lakini uhusiano wao umekua wa mashaka siku za karibuni.

Ramaphosa anasema atapambana na rushwa jambo ambalo kwa Zuma limekua kama mzigo.

Hivi ni vitu vichache ambavyo vinaweza kujitokeza kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2019:

1.Zuma kutimuliwa
Muhula wa Rais Zuma kuiongoza Afrika Kusini unaisha mwaka 2019
Image caption
Muhula wa Rais Zuma kuiongoza Afrika Kusini unaisha mwaka 2019
Chama cha ANC kitapendelea kuona kiongozi mkuu wa chama akiwa pia Rais wa nchi, jambo ambalo kama litatokea litamfanya Zuma kuachia ngazi ama kutimuliwa.

Hii itafungua njia kwa Ramaphosa kuchukua madaraka na kujaribu kurudisha imani ya wengi iliyopotea juu ya chama hicho kikichukuliwa kama cha kifisadi, huku asilimia 62 ya uwezo wa chama hicho ukiwa mashakani.

Lakini jambo hili linatajwa kuwa la hatari kwa sababu linaweza kusambaratisha chama.

Cyril Ramaphosa ndiye kiongozi mpya wa chama cha ANC

Chama cha ANC cha Afrika Kusini kumchagua kiongozi mpya

Baadhi ya viongozi wakuu wa ANC akiwemo Rais mpya wa chama na katibu mkuu wake wanaweza pia kumtimua.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Rais kufukuzwa ndani ya chama , mwaka 2008 Rais wa wakati huo Thabo Mbeki alitimuliwa baada ya Zuma kuingia madarakani kama Rais wa chama.

Uamuzi wa kumfukuza Zuma unaweza kufanywa na kamati kuu ya ANC ambayo ina mamlaka makubwa ndani ya chama.

2.Zuma kujiuzulu
Rais wa zamani Thabo Mbeki alijiuzulu baada ya kupata upinzani mkali ndani ya chama
Image caption
Rais wa zamani Thabo Mbeki alijiuzulu baada ya kupata upinzani mkali ndani ya chama
Jambo jingine ambalo limetajwa na mchambuzi wa masuala ya siasa wa Afrika Kusini Somadoda Fikeni ni uwezekano wa viongozi wakuu wa chama kumshawishi Zuma kuachia madaraka.

''Viongozi wa ANC wanaelewa gharama watakazoweza kuzipata iwapo Zuma atakuwa madarakani mpaka uchaguzi ujao''alisema.

''Kuna uwezekano wakapoteza kura nyingi ama kushindwa kabisa,'' Aliongeza.

''Kwa maana hiyo uongozi huo unaweza kuongea nae kwa amani na kumshawishi kuachia ngazi kwa manufaa ya chama'',alisema Fikeni.

3.Zuma kusalia madarakani.
ANC ni chama kikongwe zaidi Afrika Kusini
Image caption
ANC ni chama kikongwe zaidi Afrika Kusini
Kuna wale wanaoamini kuwa litakua jambo lisilo na busara kwa Ramaphosa kumfukuza ndani ya chama Rais Zuma kwa sababu inaweza pelekea kukigawanya kabisa chama hicho zaidi na kuharibu mipango yao juu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2019.

Badala yake wanaona ni vyema kwa Ramaphosa kujiimarisha zaidi na kuwa karibu na Zuma ili kuongeza nguvu ya kushinda uchaguzi wa 2019.

Kipi kitakachotokea? Bila shaka huu ni wakati mgumu kwa Zuma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad