JE Ronaldo Ndiye Mchezaji Bora Kuwahi Kutokea?

Kuna mtu ameniuliza je kauli ya Ronaldo kuwa amejitangaza mchezaji bora wa dunia muda wote naichukuliaje? Nimemjibu kirahisi sana. Ndio yupo sahihi. Ameniuliza kwanini? Nikamjibu kwa sababu Ronaldo amesema. Akaniuliza tena ina maana Lionel Messi, Ronaldinho Gaucho, Pele, na Diego Maradona wamezidiwa na Ronaldo? Najua lengo lao wanazungumzia kipaji. Nikamuuliza hao uliowataja wamemzidi nini Ronaldo. Wataniambia Ronaldinho ana chenga Messi ana balaa na Pele alifunga magoli pipa zima.

Walio wengi wanachanganya mambo. Sijui kwanini wanapapatika kwa kauli hii ya Ronaldo.

Kwani Ronaldo akijiita hivo nyie kinawauma nini? Au amekosea nini? Au labda niwaulize kigezo cha mchezaji bora wa dunia wa muda wote ni nini? Kipaji na juhudi vyote ni sawa kama tu vitakupa mafanikio. Yaani Ronaldinho hawezi kuwa mchezaji bora wa muda wote kwa sababu ya Udambwi tu. Hilo pekee halitoshi kuwadharau wenye juhudi na mafanikio. Duniani hakuna kigezo cha ni nani bora zaidi ya nani hasa wachezaji waliocheza nyakati tofauti na ligi tofauti. Ronaldo ana sababu zake za kujiita hivo. Kama hutaki basi jiite wewe ndo mchezaji bora au andaa tuzo zako umtaje mchezaji wake bora.

Ronaldo anaona ana mafanikio ambayo wengine hawana. Hakuna mchezaji aliyewazidi wachezaji wote duniani kila kitu. Soka ni kama choo kila mwenye divi anaingiamo, uwe unaendesha uwe una magogo au unaenda kukojoa wewe una haki ya kuingia. Ronaldo anafahamu alichomzidi nacho Pele, na anaona kipo ambacho maradona hawezi kujivunia. Yapo aliyozidiwa na wenzake na yeye ana rekodi zake ambazo hao mnawaona bora hawanusi. Kwanza ni mchezaji pekee duniani ambaye amefunga kila dakika. Ni mchezaji pekee aliyefunga magoli zaidi ya 50 kwa mwaka ndani ya miaka 6. Mchezaji wa kwanza na pekee aliyefikisha magoli 100 ya UEFA.

Ronaldo ni mchezaji aliyeingia kwenye tuzo za Ballon D Or mara 10 yeye na Messi. Mchezaji aliyebeba makombe yote aliyoshiriki akiwa na klabu mbili tofauti. Mpaka sasa hivi kwa taarifa yako Ronaldo ana Record 96 zake yeye kama yeye ambazo amewazidi hao magwiji. Tena usisahau hakuna aliyefikia rekodi yake ya Hat trick ndani ya la liga. Sijui kwanini mnakuwa na pua ndefu hata kwenye vitu ambavyo havina harufu nzuri. Kwanini uwe na wivu na kauli za watu? Ukimuona mbwa amekuja kwenye sherehe usimfukuze huenda amefuata ulichofuata. Muacheni Ronaldo ajisifu ana haki hiyo.

Msishushe Ronaldo kisa watu mliohadithiwa.  Ndugu zangu kinyesi cha kale hakipimwi maradhi. Hebu tusing’ang’anie kiporo cha piza tena za juzi kisa hamtaki mihogo ya sasa. Ronaldo ni mchezaji bora duniani wala hupaswi kuongea taratibu. Kama nyie hamtaki kuthamini alichofanya kwanini asisifie mtarimbo wake? Mwanaume sifia mzizi wako ili watu wasichukue mti wako.

Kila aliye bora na asimamie ubora wake. Mwanaume mwenye uchu wa mafanikio hasifii mali za mwanaume mwingine ila hujigamba kwa kile alicho nacho. Hakuna kigezo cha nani ni bora hivyo kila mtu apambane na hali yake
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad