Jerry Muro Ajipima Uwezo na Chadema “Mimi Jerry Muro Mmoja ni Sawa na Wabunge 10 wa Chadema"

Jerry Muro  Ajipima Uwezo na Chadema “Mimi Jerry Muro Mmoja ni Sawa na Wabunge 10 wa Chadema"
Aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC, Jerry Muro amesema kutokana na uwezo wake katika mambo mbali mbali anaweza kujilinganisha na wabunge 10 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katika mahojiano na kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm, Jerry amesema kutokana na uwezo wake suala la ubunge kwake ni jambo rahisi tu sawa na kubofya button.

“Mimi Jerry Muro mmoja ni sawa na wabunge 10 wa Chadema, nimewazidi kifikra, kinguvu, kipesa, maadili, kihoja na mambo mengine mengi sana” amese Jerry.

Katika hatua nyingine Jerry amesema mwaka 2020 si ajabu kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Edward Lowassa wakirejea katika Chama cha Mapinduzi (CCM).
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Swadakta J.Muro.
    Unacho sema ni Kweli. Kuna wakati tulikuwa na Go..less lilivyotajwa Jina lako tu. Jamaa alipaliwa.
    mazungumzo livyo kuwa yanaendelea.. Ilibidi aage na kutoweka.
    Kweli kihoja hawakuwezi.
    Ki maadili Hawakuwezi.
    kimpangilio Hawakuwezi.
    Ki utumizi wa Akili Hawakuwezi.
    Ki Uzalendo Hawakuwezi na wala Hujajiweka Kikanda.

    Jerry. Big Uppppp Bro.
    Hawa wana vioja tunawajua na wanajijua. Wote wako njiani... tunahesabu hatua zao tu hawako mbali.
    Hapa kazi tu.... Tanzania Kwanza.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad