Jeshi la Polisi la Tanzania, Rwanda Waungana Ili Kupambana na Uhalifu

Jeshi la Poliusi la Tanzania, Rwanda Waungana Ili Kupambana na Uhalifu
TANZANIA na Rwanda Zimeunganisha nguvu kupitia Majeshi yao ya Polisi chini ya wakuu wake IGP Simon Sirro wa Tanzania na RNP Emmanuel Gassana wa Rwanda ili kupambana na uhalifu, ujangili na kuangalia namna ya kutatua matatizo ambayo inazikumba nchi hizo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Gassana amesema kuwa lengo ni kushirikiana kutokana na changamoto ambazo zinatokea katika nchi ikiwemo kuongeza nguvu, teknolojia, vifaa na kuongeza uzoefu wa matumizi ya vifaa.
Kwa upande wake, IGP Sirro amesema kuwa kwa ushirikiano huo ambao unafanyika kwa kuangalia nini ambacho kinatakiwa kufanya na maarifa ambayo yatatumiwa ili Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake kwa usahihi na kupunguza uhalifu na endepo mtu akijiingiza kwenye uhalifu anaweza kupoteza familia yake na kuishia pabaya.
“Wenzetu Rwanda wako mbele katika matumizi ya teknolojia, hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo watatuelekeza na tutapata uzoefu katika kupambana na wahalifu wa mitandaoni ambao wamekuwa wakiwasumbua raia. Sisi pia tuna uzoefu wa mambo mengi ambayo wenzetu Rwanda watajifunza kutoka kwetu,” alisema Sirro.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naaanza kuamini waliyotabiri manabii naona kabisa kila lililotabiriwa linaanza kutokea eeeMungu tusaidie

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad