Kabla ya 40 ya Marehemu Ndikumana...Irene Uwoya Achafua Hali ya Hewa na Picha za Faragha

WHY? Hata kabla ya siku 40 baada ya kifo cha aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ au ‘Ndiku’, staa wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya, anadaiwa kuchafua hali ya hewa na kuwafanya watu wake wa karibu kushindwa kuamini alichokifanya.

Jana, Jumapili, picha za Uwoya akiwa kimahaba kitandani na mwanaume, zilichafua upepo kwenye mitandao ya kijamii ambapo mwanamama huyo alinangwa kuwa, angalau angesubiri mumewe huyo aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume, atimize siku 40 kaburini ndipo ajiachie.

Picha hizo zilisambaa wakati Ndikumana akitimiza mwezi mmoja na siku mbili tu kaburini kwani alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 15, mwaka huu akiwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Rayon ya Rwanda. Gazeti hili lilifanya uchunguzi juu ya picha hizo ambapo kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Uwoya, picha hizo zilisambaa ikiwa ni mwendelezo wa ‘kutafuta kiki’ ya tamthiliya mpya ya msanii huyo baada ya ile kiki yake na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ ya kufunga ndoa kudaiwa kubuma.

Jana, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Uwoya ‘fizikali’ kwa kufika nyumbani kwake maeneo ya Sinza-Mori, Dar, lakini likamkosa. Alipoendewa hewani, simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) hakujibu
STORI: Imelda Mtema, Dar

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo magu umetoa tamko tu kuwa linakukera hila ungeenda mbali zaidi takukuru wangechunguza hawa wapuuz

    ReplyDelete
  2. Tatizo magu umetoa tamko tu kuwa linakukera hila ungeenda mbali zaidi takukuru wangechunguza hawa wapuuz

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad