Kaka wa Wa Lissu Kujibu Barua ya Bunge Kuhusu Stahiki za Lissu

Kaka wa Wa Lissu Kujibu Barua ya Bunge Kuhusu Stahiki za Lissu
Alute Mughwai,kaka wa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, amesema anatarajia kujibu barua iliyoandikwa kwake na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai ikihoji stahiki ambazo chombo hicho kinapaswa kumpatia ndugu yake.

Akizungumza na MCL Digital, Mughwai amesema ameipata barua ambayo ataijibu na baadaye atazungumza na waandishi wa habari.

“Nilikuwa Nairobi (Kenya) ndiyo nimerejea, nitaijibu barua hiyo na nitaiwasilisha kabla ya Alhamisi halafu ndani ya siku mbili hizi nitawaeleza kila kitu kuhusu suala hilo na maendeleo ya afya ya Lissu,” amesema.

MCL Digital ilipotaka kujua ni stahiki zipi ambazo Bunge linataka kujua kwamba ndizo anazotakiwa  kupewa Lissu, Mughwai alijibu, “Hizo ndizo danadana ila nitawajibu.”

Katibu wa Bunge, Kagaigai alimwandikia barua Mughwai Novemba 27,2017 akimtaka alieleze ni stahiki zipi ambazo ndugu yao anastahili apewe na Bunge.

Kagaigai alieleza kuhusu barua hiyo siku mbili baada ya Lissu kuhoji sababu za Bunge kutojihusisha na matibabu yake tofauti na sheria zinavyotaka.

Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikopelekwa tangu Septemba 7,2017 aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari kwenye makazi yake eneo la Area D mjini Dodoma.

Kauli ya Lissu ilikuwa mwendelezo wa ya awali iliyotolewa na Mughwai aliyesema alishaiandikia ofisi ya Bunge kutaka ilipie gharama za matibabu ya mbunge huyo.

Katika mahojiano na Mwananchi hospitalini jijini Nairobi, Lissu alisema alimweleza Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alipokwenda kumjulia hali kuwa, “Bunge liko wapi” kutokana na kutofanya juhudi za kwenda kumuona tangu alazwe.

Pia, alieleza kushangazwa na kitendo cha chombo hicho kutogharimia matibabu yake licha ya kuwa ni stahili yake kisheria iwe anatibiwa ndani au nje ya nchi.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lissu hana Haki ya Kuuliza Bunge liko wapi? .....Bunge liko Dodoma
    Yeye haja ajiriwa na Bunge ila amefikishwa Bungeni kuwawakilisha Waliomchagua kuwa ndiyo sauti yao.(ambayo wangeweza kunchagua yeyote wamtakae ili awamalizie kero zao za maisha)
    Kama wamekuchangia posho ya ya siku ile ni Ubinadamu wao.. Na kama wamekuja kukutembelea pia ni Ubinadamu wao... Si wa Kuuliza Bunge liko wapi. Ulikuwa unategemea Bunge liwekewe turubali hapo?

    Huyu ndugu anaezungumziwa hapa... Mwajiri wake ni Nani na anaweza kuzungumza kwa sheria Ipi inayo mpa fursa hiyo?
    Hizo salamu anazotaka kuzijibu zinatoka kwa nani kwenda kwa Nani? Na kwa Misingi Ipi?
    Huko alipokwenda kujitibia alikwenda baada ya Uamuzi wa Nani na Kwa Matarajio au Makubaliano ya Nani?

    Je Hospitali ya Dodoma waliridhika kuwa hawana uwezo wa Kumtibu mgonjwa huyo wakati akihitaji matibabu? Na kuweza kutoa referal kwa Hospitali ipi? na nani alithibitisha Hilo?

    Waajiriwa wa Bunge mpaka sasa idadi yao ni Wangapi ambao wanapata stahiki ikiwemo Bima ya Uuuguzi na Uganguzi?

    Msijichanganye na Kutuchanganya.
    Maji yanaitwa Maji na Soda ni Maji ila imetiwa Rangi na Sukari ndiyo tofauti yake.
    Sasa Hii ni Soda au Maji?
    Bado mpaka makachero wetu waliotumwa na IGP amewatolea nje na Kutotoa Ushirikiano.

    Tunakuombea Dua upone ili urudi Muhimbili kwa ukaguzi wa afya yako na ahueni yako.

    Hii si Siasa wala Kuhusiana.... Na msilipeleke Huko kwenye siasa Uchwara na Maigizo ya kudandia.

    ReplyDelete
  2. mi nafikiri hawa jamaa wa lisu walitakiwa wafikiri kwanza kabla ya kutenda walijiona wao ndio kila kitu hatupandi yale yaliyomtokea lakini hawakutafakari kwa kina walipokuwa najiondoa kibabe nchini na kingine kule waliko nani aliwapeleka wakati utaratibu unajulikana na kibaya walishauriwa walikataa sasa inakuwaje tena?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad