Kampeni ya Kuhamasisha Tohara kwa Vijana wa Kiume Kuanzishwa

 Kampeni ya Kuhamasisha Tohara kwa Vijana wa Kiume Kuanzishwa
Vijana wa kiume wametakiwa kuwa tayari kufanyiwa tohara ili kukabiliana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Sauti ya Mama Afrika (Samofa), Thabitha Bughali alisema jana kuwa, wameanza kampeni kuhamasisha tohara kwa vijana walio na miaka 12 katika shule za msingi na sekondari kwa lengo la kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Alisema katika kampeni hiyo wanawalenga vijana wa umri huo kutokana na changamoto ya utandawazi katika jamii na wengi wao kujihusisha na ngono wakiwa na umri mdogo na hivyo kuwa katika hatari ya kupata Ukimwi.

Bughali alisema kuanzia Januari hadi Julai, wamefanya uhamasishaji kwa vijana 500 katika baadhi ya shule za kata za Utengule Usongwe na Nsalala, Mbeya Vijijini.

Mkazi wa Itende, Joshua Seme alisema ili Serikali ifanikiwe katika kampeni ya tohara, elimu zaidi inapaswa kutolewa maeneo ya vijijini ambako kuna changamoto ya idadi kubwa ya wanaume wasiofanyiwa tohara.

Desemba 6, mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla aliwaagiza waganga wakuu wa hosptali mkoani hapa kufanya kila linalowezekana ili kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Agizo hilo alilitoa katika kikao cha afya mkoa kilichohusisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu na wataalamu wa afya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad