Katibu wa Bunge Ahoji Stahiki za Tundu Lissu

Katibu wa Bunge Ahoji Stahiki za Tundu Lissu
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema amemwandikia barua kaka wa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, akimtaka alieleze ni stahiki zipi ambazo ndugu yao anastahili apewe na chombo hicho.

Kauli hiyo inayoweza kuibua malumbano mapya katika matibabu ya mwanasheria huyo mkuu wa Chadema, imetolewa siku mbili baada ya Lissu kuhoji sababu za Bunge kutojihusisha na matibabu yake tofauti na sheria zinavyotaka.

Lissu yuko Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anatibiwa tangu Septemba 7 aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana wakati waki ndani ya gari lililoegeshwa nje ya makazi yake mjini Dodoma.

Kauli ya Lissu ilikuwa ni mwendelezo wa kilio kilichotolewa awali na ndugu yake, Alute Mughwai Lissu ambaye alisema alishaiandikia ofisi ya Bunge kutaka ilipie gharama za matibabu ya mbunge huyo.

Katika mahojiano na Mwananchi hospitalini jijini Nairobi, Lissu alisema alimwambia Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ahoji “Bunge liko wapi” kutokana na kutofanya juhudi za kwenda kumuona tangu alazwe takriban miezi mitatu iliyopita.

Pia alieleza kushangazwa na kitendo cha chombo hicho kutogharimia matibabu ambayo anastahilki kisheria iwe anatibiwa ndani au nje ya nchi.

Lakini jana, alipoulizwa kuhusu hatua waliyofikia baada ya kupokea barua ya familia hiyo iliyotaka Bunge lizingatie haki za msingi za ndugu yao, Kagaigai alionekana kutaka maelezo kutoka kwa familia.

“Sisi tumewajibu hizo haki ni zipi kwa sababu kuna allowance (posho) kuna mshahara zote hizo ni haki za mbunge. Hajajibu haki anazoongelea ni zipi,” alisema Kagaigai ambaye alimtaka mwandishi wa Mwananchi asimrekodi sauti yake na baadaye kuandika maelezo hayo katika daftari lake.

Kigaigai alisema barua hiyo imeandikwa na Bunge Jumatatu (Novemba 27) na kwamba bado wanasubiri majibu kutoka kwa Alute kuhusu haki anazotaka Bunge izingatie.

Alipotafutwa azungumzie majibu hayo ya katibu wa Bunge, Alute ambaye kitaaluma ni wakili wa kujitegemea, alisema hajapata barua hiyo ya ofisi ya Bunge.

“Mpaka sasa (saa 7:00 mchana) sijapokea barua yoyote.”

Kuhusu haki hizo, Alute alisema kama ambavyo alizungumza huko nyuma kwamba sheria inamtambua Lissu na hivyo anatakiwa agharimiwe matibabu yake.

“Lissu si wa kwanza au wa mwisho kutibiwa nje. Matibabu ya mbunge kwani ndio yanaanzia Lissu?” alihoji.

“Yanatambulika kisheria kwa hiyo sijajua hiyo barua imetutaka kufanya nini. Ngoja tuisubiri.

“Hivi (aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini-CCM, marehemu) Leonidas Gama alivyokwenda India, alijipia au aligharamiwa na Bunge?”

Katika mahojiano kati na Mwananchi jijini Nairobi, Lissu alisema kwa wadhifa wake wa ubunge na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni anatambuliwa na sheria za Tanzania hususan Sheria ya Uedeshaji wa Bunge na kugharamiwa matibabu si hisani bali ni stahiki zake.

Alisema sheria hiyo inaeleza mbunge anapoumwa atapata matibabu pamoja na gharama nyingine kutoka bungeni pamoja na mtu anayemuuguza ambaye hulipwa nusu ya posho ya mbunge ili kumudu gharama za maisha.

Alisema hilo hufanyika baada ya mgonjwa kuwa amelazwa nje ya eneo la Bunge, akimaanisha Dodoma na bila ya kujali anatibiwa Dar es Salaam, Afrika Kusini, India Marekani au Kenya.

Lissu alisema Spika wa Bunge, Job Ndugai anajua kwamba aliumizwa na ndiyo maana aliwahi kulitangazia Bunge na akaendesha shughuli ya kumchangia ingawa alishangazwa na ukimya wa yeye kutopewa stahiki zake na kuahidi akitoka atazipigania kwani ni haki zake.

Septemba 21, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga kuhusu gharama za matibabu ya Lissu, alisema Serikali haijashindwa wala haijakataa kumhudumia.

“Lissu ni Mtanzania na ni mbunge,” alisema.

“Hata sasa hivi anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi, lakini kidogo tunaona kunafanyika mambo tusiyoyaelewa kama dhamira ya kufanyika kwa mambo hayo.

“Muwaeleze Watanzania na familia kwamba Serikali iko tayari kumhudumia Lissu popote anapotaka kupelekwa duniani iwapo tutapata maombi rasmi kutoka kwa familia.”

Ufafanuzi wa Waziri Mwalimu ulitofautiana na ule alioutoa Spika wa Bunge, Job Ndugai Septemba 15 bungeni mjini Dodoma wakati akijibu tuhuma za wabunge, hususan wa upinzani waliodai Bunge limeshindwa kumgharamikia Lissu.

Ndugai alisema baada ya kueleza kwamba utaratibu wa bima wanayotumia ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni wa kutibiwa katika hospitali za Serikali.

“Sisi wote tuna bima pamoja na mawaziri na bima yetu inafanana na ni NHIF. Bima yetu tunatibiwa katika hospitali hii yetu ya mkoa au hospitali nyingine za Serikali, rufaa yetu ni Muhimbili. Baada ya hapo ni kupelekwa India Hospitali za Apollo,” alisema Spika.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lissu Ni lazima arudishwe Muhimbili. Aendelee na matibabu kama Watanzania wenzake. Lissu Hana tofauti Goddluck mlinga au Kingwendu. Ikiwa Mzee Majuto Mke WA Raisi wametibika hapa hapa. Kiasi PIA no mmoja wapo na anastagili kupata utabibu kama unahitajika hapa MOI Ni kitengo teule katika fani na umahiri WA uuguzi. Ulimuuliza nimi nani alikuoeleka huko uliko na kea matarajio yepi walivyo jipanga kumudu hili? Msituchanganyie mada na maamuzi ya majuto mjukuu. Na msiendelee kutukanisha madaktari wetu na hospyali zetu na huruma Mtanzani nchi Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Kama Ummy Mwalimu alikosea Majibu ajili ya Ushinikizo wa Wanasiasa. Basi hiyo ni mawazo yake na hakuwa mzungumzaji wa Serikali au kujibu swali la Kisiasa.
    Sasa Ya lissu msiyafanye kuwa ni yaKisiasa.
    Lissu ni Mtanzania kama Watanzania walio wengi .
    Ameshambuliwa na Majambazi kama Nassiri anavyo dai mbwa wake wawili wameuliwa.
    Lissu ashauriwe na yeye kuweka mbwa 4 na arudishwe Muhimbile Kuchunguzwa Zaidi na Kupata Matibabu kama yanahitajika.
    na kuangalia maendeleo yake. Na ikibidi muhimbili ikiwa wanaona kuna hitajika zaidi.
    Hatua stahiki zitafatwa na Hatimae kupelekwa India kama ilivyo kawaida yetu.

    Ushauri ni kwa haraka Lissu arudishwe Hospitali ya Rufaa Muhimbili Haraka Sana.
    Unless waliompeleka huko wanajua na kukidhi mahitaji ya huko ikiwemo kujikimu kwa walioandamana nae na malipo yanayojitokeza huko na wanaomtembelea pia iwe ni kwa nauli ni malipo binafsi.
    Zetu juu yake ni Dua tu. Kama ni mchango wa Wabunge tulifanya na tukatoa posho yetu ya Siku.
    Ile ilikuwa ni Kwa Ridhaa yetu na siyo Wajibu au stahiki. Hata Freeman analijua hilo .
    Plese DO NOT Politicise this .......

    ReplyDelete








  3. Watanzania Sisi Wazalendo Tunajitahidi Kuboresha Afya na Uuguzi... Lissu usitutukanishe angalia hii "
    "KAIMU Balozi wa Marekani nchini, Dk Inmi Patterson amesema Serikali ya Marekani inaona fahari kufanya kazi na Watanzania huku ikiunga mkono jitihada za wananchi kujenga Tanzania yenye amani, ustawi, usalama na afya.

    Alisema hayo katika ziara yake mkoani Mwanza Novemba 26 hadi 28, mwaka huu, iliyolenga kukuza uelewa wa wananchi kuhusu jitihada zinazofanywa na Marekani kujenga uwezo wa Watanzania katika kujenga jamii zenye afya, kukuza uchumi wa jamii na mkoa na kusaidia katika elimu.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Kaimu Balozi aliyasema hayo akiwa katika Shule ya Wauguzi ya Askofu Anthony Mayalla iliyopo katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

    Katika shule hiyo, wauguzi wa Kimarekani wanafanya kazi na kuwafundisha wenzao wa Kitanzania mbinu za kuwahudumia watoto wachanga na akina mama waliojifungua kama sehemu ya mpango wa ubia wa kutoa huduma za afya duniani.

    “Uhusiano wetu mkubwa unaakisiwa na ushirikiano wa kina baina ya nchi zetu na nina imani kuwa, tutaendelea kuimarisha uhusiano huu wa kihistoria tunapoendelea kusaidiana,” alisema."


    Sasa kurudi kwako ni Hiari yako.
    Lakini usikae ukategemea Mimi niweke Sumni Yangu au Ya Mlipa Kodi Wangu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad