Kigwangala Atoa Viwango Vipya vya Leseni ya Biashara

Kigwangala Atoa Viwango Vipya vya Leseni ya Biashara
Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii kwa wafanyabiashara na wadau wa sekta hiyo wakiwemo waongoza watalii.

Mapendekezo hayo yamewasilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu, kwenye mkutano na wadau wa Utalii Jijini Arusha ambao pia umehudhuriwa na Waziri wa wizara hiyo Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Katika mapendekezo hayo mapya, wajasiriamali wadogo katika sekta hiyo wenye gari moja hadi magari matatu ya watalii wamepata nafasi ya kutambulika ambapo watatakiwa kulipa ada ya leseni ya dola za Kimarekani 200 sawa na Shilingi  laki 450,000/=, tofauti na awali ambapo walilazimika kulipa Dola za Kimarekani 2,000.

Kwa upande wa wafanyabiashara wenye magari kuanzia manne hadi kumi imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 2,000, wenye magari 11 hadi 50 Dola za Kimarekani 3,000, magari 51 hadi 100 Dola za Kimarekani 10,000 na magari 100 na kuendelea Dola za Kimarekani 15,000.
Kwa wafanyabiashara ambao sio Watanzania wenye magari 10 hadi 30 imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 10,000, magari 31 hadi 100 Dola za Kimarekani 15,000 na magari 101 na kuendelea Dola za Kimarekani 20,000.
























Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad