Kimenuka Kanisa la Anglikana Wamtaka Askofu Mnung'a Kurudisha Milioni 8 Baada ya Kuuza Kiwanja cha Kanisa

Kimenuka Kanisa la Anglikana  Wamtaka Askofu Mnung'a Kurudisha Milioni 8 Baada ya Kuuza Kiwanja cha Kanisa
Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam imemtaka aliyekuwa ofisa ardhi kanisa hilo Kanda ya Kinondoni, Askofu Oscar Mnung'a kurudisha fedha takriban Sh 8 milioni anazodaiwa baada ya kuuza kiwanja cha kanisa hilo kilichopo Pegwa Kijiji cha Zinga Bagamoyo.

Shamba hilo lililokuwa na miti na matunda linadaiwa kuuzwa mwaka 2013 kwa shirika mojawapo la umma (jina limehifadhiwa) baada ya mchakato wa tathimini kukamilika.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Desemba 15 kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es  Salaam, Yohana Sanga amesema Askofu Mnung'a aliuza kiwanja chenye ekari tano bila lakini hakuweka fedha katika akaunti ya kanisa.

Sanga amesema wamegundua hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa wenyeji wa eneo hilo ambao walithibitisha kuuzwa kwa shamba hilo na askofu huyo.

"Baada ya kufutialia kwa kina dayosisi imebaini Askofu Mnung'a alililipwa fedha hizi lakini hakuziwasilisha katika akaunti ya kanisa kama ilivyopaswa. Kwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa nyumba 10 wa eneo hilo askofu huyo amehusika moja kwa moja katika mchakato huu," amesema Sanga katika taarifa  hiyo.

Kwa mujibu wa Sanga, Askofu wa Mnung'a hivi yuko dayosisi ya Newala mkoani Mtwara na wanamtaka kuzirudisha fedha hizo na wameamua kutoa taarifa kwa umma baada ya kuona malalamiko ya waumini yanazidi.

Akijibu tuhuma hizo, Askofu Mnung'a alikana na kuhusika na uuzwaji wa kiwanja hicho na kuwataka viongozi wa dayosisi kuwatafuta wahusika wakuu waliouza.

"Katika ile dayosisi kuna matatizo pale hivyo, wanataka kunichafua mimi kwa kunipandikiza mambo yasiyonihusu. Nawaambia wapambane na hali zao mimi simo huko," amesema Askofu Mnung'a.

Askofu Mnung'a aliwataka viongozi  hao wa Dayosisi  ya Dar es Salaam  kuonyesha vielelezo vinavyoonyesha kuwa yeye  alihusika katika mchakato huo wa uuzaji wa kiwanja bila kuwasilisha fedha  katika akaunti ya kanisa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad