Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ametoa lawama kwa wasomi nchini akidai wamekuwa wakikaa kimya hata pale wanapoona masuala ya Taifa hayaendi sawa.
Mchungaji Msigwa amesema hayo wakati wa mjadala uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) wakati wa kongamano kujadili kitabu kinachohusu miaka 70 ya kusaka demokrasia kwa nchi za ukanda wa Maziwa Makuu kilichoandikwa na Profesa Gaudence Mpangala wa chuo hicho.
“Kwanza nimpongeze Profesa Mpangala kwa kuja na utafiti huu ambao unaonyesha hali ya kidemokrasia nchini bado iko chini, nchi hii inawategemea ninyi wasomi ili iweze kusonga mbele, lakini kwa bahati mbaya mmetuachia sisi vipofu ndio tunaowachaguliwa njia ya kupita,” amesema Mchungaji Msigwa.
Amesema, “Upo usemi nimekuwa nikiutumia hata bungeni ‘akili ndogo kuongoza akili kubwa’ na leo hapa niwaeleze kuwa licha ya kuwa Taifa linawategemea, ninyi ndio mnaofanya tafiti bado mmeacha sisi wenye akili ndogo kuwachagulia ngoma ya kucheza nanyi mnakubali kuicheza hata pale mnapoona Taifa linatumbukia shimoni,” amesema.
Mchungaji Msigwa amewataka wasomi kutimiza wajibu wao na kuwataka kutumia elimu waliyonayo kushauri na kukosoa pale wanapoona inafaa kufanya hivyo.
Amesema hatua hiyo itasaidia Taifa kujenga misingi bora ya demokrasia inayoheshimu haki za binadamu na utawala bora na kusaidia kuinua uchumi wa nchi.
Mwandishi wa kitabu hicho, Profesa Mpangala amesema ili hali ya usawa wa kidemokrasia nchini iweze kufikiwa ni lazima kuandika Katiba mpya kwa kurejea maoni yaliyomo katika rasimu ya iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
msigwa, umeshapimwa akili wewe na wenzako wa chadema?? Ulisema atakayempokea Lowasa akapimwe akili.....hebu mkapimwe kwanza, mtuletee majibu labda tutawaelewa.....kinyume na hapo, ni sawa na kumpigia 'gitaa' mbuzi....hatuwaelewi!!!
ReplyDeleteWe hapo juu badala ya kuongelea haya yanayojadiliwa ambayo ni mazito sana katika taifa unaongea pumba. Unamkashifu mtu. Toa hoja kuhusiana na mjadala. Sijui ni msoni au mtu tu wa barabarani .huonyeshi kama unakisomo chochote kwenye jibu lako. Unatoa porojo kama wengi watoao porojo majukwaani. Ni kilaza mmojawapo hata commonsense huna. Ni kubwata kila kukicha na kubwatuka. Kama unauwezo wa kufikiri andika hoja. Huna hoja funga domo.mnaaibisha nyinyi mambumbumbu.
ReplyDeleteMbumbumbu ni wewe, Mdau anazungumza alicho zungumza Musigwa akili na Akili Timamu.
DeleteNa kwa hivi sasa ni lazima apimwe mkojo. Nazungumza Pumba na Hajielewi kama Wewe Na Zito.
Wenye Akili zao wote wamesha shika njia . Je wewe unagoja NINI . Ruzuku hupati inachukuliwa na Vilaza kama Wewe na Wanakusahau wala Huulizi.
Hapa Kazi Tu.
Msigwa Lemo ameshamwambia yuko njiani anaogopea M/kiti wake asipate shtuko na mapigo ya moyo kuchanganyika kama hali ilivyo sasa.
Shauri yenu. Ukweli mnaujua na Utabaki kuwa Ukweli.