Kiongozi Upinzani Amuangukia Rais Aomba Msaada wa Milioni 60

Kiongozi Upinzani Amuangukia Rais Aomba Msaada  wa Milioni 60
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda amepiga goti na kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli aweze kukisaidia chama chake cha Ada Tadea milioni 60 ili waweze kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge unaotegemewa kufanyika mapema 2018


Shibuda ameomba hilo leo Disemba 18, 2017 akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema endapo Rais akiwasaidia milioni 20 kwa kila jimbo hivyo wataweza kushiriki uchaguzi wa marudio wa Ubunge katika majimbo matatu ambao unategemewa kufanyika Januari 13, 2018.

"Nakuomba utombee kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli atutazame tupate ruzuku vyama visivyo pata ruzuku ili tuwe sawa na wale unaowapa ruzuku lakini hawapendi kushiriki katika masuala ya uzalendo na utaifa, lakini chonde chonde nakuomba utuombee" alisema Shibuda

Baada ya maombi yake hayo Rais Magufuli alimuuliza kama yeye na chama chake atashiriki katika uchaguzi wa marudio wa wabunge ndipo hapo aliporudi na kuomba apewe milioni 20 kwa kila jimbo.

"Naomba nisaidie milioni 20 kwa kila jimbo ili niwezeshe kwenda kugombea kwa hiyo kwa majimbo matatu tusaidie chama milioni 60 kwa sababu unaowapatika ruzuku hawakwenda kushiriki" alisisitiza Shibuda.

Baadhi ya Vyama vya siasa vya upinzani nchini Tanzania kikiwepo CHADEMA, CUF, TLP, CHAUMMA pamoja na ACT Wazalendo vimejitoa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa marudio wa nafasi ya Ubunge ambao unategemewa kufanyika Januari 13, 2018 kwa kile walichodai kuwa uchaguzi wa madiwani uliofanyika karibuni haukuwa wa haki na ulitawaliwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na kanuni za uchaguzi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad