Kitua cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 8,157 ikiwemo familia ya msanii Nguza Viking.
Pamoja na pongezi hizo LHRC, imesema itaendelea kumuomba Rais Magufuli abadili baadhi ya sheria ikiwemo kuondoa sheria inayotoa ruhusa ya adhabu ya kifo..
“Tunampongeza Mh. Rais Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 61 kati ya wafungwa 522 waliohukumiwa kunyongwa”. LHRC wameandika kupitia ukurasa wao wa Twiiter.
Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
LHRC imeongeza, “Tunamsihi Mhe. Rais kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta sheria zinazoruhusu uwepo wa adhabu ya kifo na kuifanya hukumu ya kifungo cha maisha kuwa adhabu mbadala”.
Katika msamaha huo Rais pia amemsamehe mzee Mganga Matonya ambaye ana miaka 85 akiwa amekaa gerezani miaka 37 pamoja na miaka saba aliyokaa mahabusu wakati akisubiri hukumu yake hivyo kufanya afikishe miaka 44 gerezani.
Magu Baba..!!!
ReplyDeleteMungu akuwe na akulinde.
Mlio achiwa tunakuombeni chonde chonde Msimwangushe Raisi wetu na Imani yakw Juu yenu.
Rudini Uraiani na muwe Wazalendo na Raia wema. Nchi yetu ni Salama na tunahitaji Amani yenu Uraiani kwetu.
Karibuni sana muungane na Familia zenu na kuwaondolea dhiki za kowakosa kwa muda wote mliokuwa hamko nao.
Iwe ni Furaha na Amani kwenu.
karibuni na tujenge Taifa kwa pamoja.
Na tufanye kazi kwa bidii kweli kwelinchi inakuhitajini katika uzalishaji na kulitumikia Taifa. kumbukeni hii ni awamu ya
HAPA KAZI TU NA SI VINGINEVYO.
ASANTE BABA JPJM. Watakuelewa tu.