WABUNGE wa CHADEMA, Peter Lijualikali (Kilombero) na Suzan Kiwanga (Mlimba) pamoja na washtakiwa wengine 37 ,jana wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kusikiliza maombi ya kupatiwa dhamana kwenye kesi inayowakabiri.
Mahakama imetatoa uamuzi huo saa 9 alasiri leo baada ya mabishano ya kisheria juu ya dhamana za Wabunge wa CHADEMA, Peter Lijualikali na Suzan Kiwanga na washtakiwa wengine 36.
Itakuwambukwa kuwa, Washtakiwa hao kwa ujumla hao wanakabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kuchoma moto ofisi za serikali ya Kijiji cha Sofi, wilayani Malinyi katika uchaguzi wa mdogo wa madiwani uliomalizika hivi karibuni mkoani Morogoro.
Upande wa mastaka ukiongozwa na Sunday Hyera na Edga Bantulaki uliwasilisha maombi mahakamani hapo kupingwa watuhumiwa kuachiwa kwa dhamana kwa kile kilichoelezwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo utaharibika.
Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Peter Kibatala ulipinga mamobi hayo na kueleza kuwa kiapo hicho cha kupinga dhamana kilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria pamoja na kukosekana kwa uthibitisho wa mtu aliyeandika kiapo hicho.
Baada ya pande zote mbili kuvutana kwa hoja za kisheria kwa takribani saa 2, hakimu Ivan Msack aliahirisha kesi hiyo kwa muda na baadaye ndipo ikaamuriwa waachiwe kwa dhamana.