Lipumba Apigwa Stop Kufanya Shughuri za CUF

Lipumba Apigwa Stop Kufanya Shughuri za CUF
Bodi ya (CUF) ambayo ipo chini ya Mwenyekiti wa (CUF), anayeungwa mkono na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba imepigwa marufuku kufanya shughuli zozote zinazoihusu Taasisi ya CUF mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa.


Naibu Mkurugenzi Uwenezi wa CUF kwa upande wa Maalim Seif, Maharagande amesema kuwa maamuzi hayo yametolewa leo Disemba 19, 2017 mbele ya Jaji Wilfred Dyansobera katika Mahakamu Kuu Dar es Salaam ambapo Jaji Dyansobera ameitaka bodi hiyo inayodaiwa kuwa ni bodi feki kutojishughulisha na kazi zozote za taasisi ya CUF.

"Mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera ameipiga marufuku bodi feki ya Lipumba kufanya shughuli zozote zinazoihusu CUF mpaka pale shauri la msingi litakapomalizika. Awali Jaji aliyatupilia mbali maombi ya Wakili msomi Ngole ya kumuomba Jaji asisome maamuzi hayo kwa madai kuwa wanakusudia kukata rufaa juu ya maamuzi ya Jaji kukataa kujitoa kusikiliza mashauri ya CUF. Jaji amesema hakuna hoja za kisheria zinazoizuia mahakama kuacha kuendelea na shughuli ilizozipanga" alisema Maharagande

Mbali na hilo Naibu Mkurugenzi Uwenezi wa CUF kwa upande wa Maalim Seif, Maharagande amesema kuwa CUF ni taasisi imara yenye viongozi makini na kudai kuwa kwa ushindi huo ni wazi kuwa CUF mpya inazaliwa muda si mrefu sana.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad