Lissu Aanza kusimama kwa Mara ya kwanza kwa Msaada wa Madaktari.

Lissu Aanza kusimama kwa Mara ya kwanza kwa Msaada wa Madaktari.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Nairobi Kenya baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana, ameanza kusimama kwa mara ya kwanza kwa msaada wa madaktari.


Taarifa kutoka Hospitali ya Nairobi imeeleza kuwa Lissu kwa mara ya kwanza ameweza kusimama kwa msaada wa Physiotherapist tangu  Septemba 7, mwaka huu alipopigwa risasi mjini Dodoma, hatua chache kabla ya kufika nyumbani kwake.

Akizungumza kutoka Hospitalini hapo, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanansheria Tanganyika (TLS), amesema "Wapendwa wote wiki iliyopita niliwataarifu kwamba  madaktari wangu wamesema nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania"

"Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa mababa cheza kama inavyoonekana, hatua inayofuata nitawajulisheni," Lissu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad