Doctor Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda kusihi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo.
Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa inlocshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa New York Marekani.
"Sasa hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu alafu mimi nisepe, nikiwa hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa Bara la Afrika, sasa ni world wide ofisi itakuwa New York, nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR, hata mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto power, veto power ziko tano kwenye umoja wa mataifa, jina langu lilikuwa projected na Urusi na mwenyewe Putin", amesema Dkt. Shika.
Dkt. Shika ameendelea kwa kusema kwamba kura ambazo alipata zilitosha kwa yeye kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa, kwani nchi tatu zilikubali jina lake kupitishwa ikiwemo na Marekani.
Mimi Naona kama Kajichanganya au .......
ReplyDeleteHela za Kutoka Thailand zimeshafika?
Shika Umetisha....!!!!!
Dokta...Usimsahau nyuma Mdada Katherin Kahabi.. Amekutoa mbali mpe hata kazi ya nyumbani huko Nyoko malekani. Maaana yake Catty ameweza kukufanya kuwa Brand by its own Right.
ReplyDeleteShika unatisha....lakini pia unatia wasiwasi uko timamu..??
Utakifazili Chuo....!!!
Utajenga Viwanda....!!!
Unakwenda Malekani..!!!
Pesa zinaluja to Tailandi...!!!
Mimi Balozi Umoja wa Mataifa..!!!
Yote haya ni yako???
Mama Kahabi Usiliwache Buzi....!!!! Kaa nae Beneti hata Wema usimpe nafasi ( Kuwa hata sekletali wake UNHCR) au hata Getini tu wewe upo upo tu.