Maandamano Ya Upinzani Yakwama Kongo

Maandamano Ya Upinzani Yakwama Kongo
Maandamano yaliyoitishwa leo na viongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, (DRC), yameshindwa kupata mwitikio mkubwa kama ilivyotarajiwa baada ya Serikali kuyapiga marufuku na kusambaza maelfu ya polisi.


Upinzani ulikuwa unajaribu kuwashawishi wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kwenye viunga vya jiji la Kinshasa na maeneo mengine ya nchi kushinikiza Rais Joseph Kabila kuondoka madarakani ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Maandamano hayo yalikuwa yanalenga pia kupinga kalenda mpya iliyotangazwa na Tume ya uchaguzi nchini humo, ambayo sasa inaonesha kuwa uchaguzi mkuu utafanyika Disemba 23 mwaka 2018.

Rais Kabila alikuwa amemaliza muda wake Disemba 20 mwaka jana kabla ya kufikiwa kwa makubaliano kati ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, na wanasiasa kuwa uchaguzi ungefanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Upinzani umeendelea kushinikiza kuwa unataka kuundwa kwa Serikali ya mpito bila ya Rais Kabila kuanzia Januari Mosi mwaka 2018.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad