Mabilioni ya Hela Yakamatwa Yakiingizwa Nchini Kinyume cha Sheria

Mabilioni ya Hela Yakamatwa Yakiingizwa Nchini Kinyume cha Sheria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema zaidi ya dola bilioni moja zimeshikwa zikiingizwa nchini kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.

Akiwa jukwaani mjini Dodoma leo wakati akizindua tawi la Benki ya CRDB, Rais Magufuli ameweka wazi kuwa amepata taarifa zaidi ya kiasi cha dola bilioni moja zimeshikwa zikiingizwa nchini kinyume na sheria kupitia uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.
“Ninapozungumza tu sasa hivi nimepata taarifa zaidi ya bilioni moja dola zimeshikwa Airport zilikuwa zinaingizwa Tanzania kwasababu Tanzania kimeshaonekana ni kichaka cha fedha za kigeni” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine Rais amezitaka mahakama za biashara nchini kuharakisha kesi zinazohusiana na kesi za mikopo ili kuwezesha Benki kuendelea kutoa mikopo. Pia ameongeza kuwa baadhi ya wakopaji hutumia fedha hizo hizo za mikopo kuchelewesha kesi, hivyo mahakama zinatakiwa kutoa hukumu kwa wakati.
“Nawahimiza wananchi kulipa madeni yao kwa wakati, dawa ya deni kulipa, na niziombe Mahakama za biashara kuharakisha kesi zinazohusu mikopo, mtu anapopelekwa amekopa na anatakiwa kuuziwa jengo lake au kufirisiwa, unachelewesha nini toa amri watu wakauze ilikusudi Benki ziendelee kukopesha wengine”, amesema Magufuli.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni nani nyuma ya hili. Na wamechukuliwa sheria gani. Ni watanzania au. Ndo wanaoharibu uchumi na kuanguka kwa thamani ya shilingi.hii ni serious matter. Mmezifanyia nini hizo pesa.

    ReplyDelete
  2. Mhhhh....hapa Kuna walakini hata kama za ....... BASI tujulishe Ni kwa minajili gani na Nia yake na madhumuni yake Ni nini... Kabla hatujaendelea na next step.
    Hongera wana usalama JK airport na IGP SIRRO.
    HAPA KAZI YU KWA MAANA HAKINA KULALA WALA KULA BINAFSI

    ReplyDelete
  3. hizi ndizo pesa zinazoingia kwenye mikono michache. Je ni malipo, hongo, ubia au ufisadi. Kuna mkono wa mwana CCM. mpinzani yeyote hawezi fanya hivi. Imetoka benki gani. Au ni ya Madawa ya kulevya, Ndo mtandao huu. Ni nani msafirishaji, nani mmpokezi, kwa mkataba gani, Wanaotawala watu ndo Hawa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ..kuna mkono wa mwana CCM... una uhakika? hebu uwe reasonable, hakuna taarifa zozote zaidi ya kukamatwa kwa hizo pesa tayari wewe unaanza kuja na upupu wako. spare us with your stupid opinions, discuss a subject matter after a thorough research short of that shut your mouth.

      Delete
  4. Hii ndiyo Neema inayo Tumia bila kuyarajia....
    Unaipiga tanchi inaingia katika kuendeleza miundo mbinu DODOMA NA. SGR.
    Hongera wana usalama na IGP Sirro

    ReplyDelete
  5. Nimepata Taarifa za Kuwa hizi prsa tegemezi zimeingia hapa ni za milionea wa nyumba za Lugumi akijulokana kama Dkt Luis Shika....itapendeza kama atapewa mwenyewe kwa nia ya malipo na kusaidia chuo.Meneja wake yupo mbioni kufanikisha hilo.
    Dkt Shika...tumeona jeuli yako...tulifikiri eree no mbanaishaji.

    ReplyDelete
  6. Yono mjipange kupokea kitita chenu.. Na Dkt Shika yuko tayari kulipia Usumbufu alioufanya na kuitokeza.
    Viwanda atavijenga na Vyuo atasaidia.
    Na huko Dodoma atajenga Hospitali ya Kimataifa....Dkt Shika Oyeeeeee, Yono Oyeeeeeeeee....!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad