Mali za CCM Zamtokea Puani Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha

Mali za CCM Zamtokea Puani Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha
Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya ambaye amesema alifunguliwa kesi nne kwa sababu ya kutetea mali za CCM na kudai wapo viongozi wa Chama na Serikali ambao wanahusika na ufujaji wa mali za Chama.


Lengai amefunguka hayo ikiwa ni siku chache baada ya Rais Magufuli kuunda kamati itakayoweza kuchunguza mali za CCM, ambapo amesema yeye kupewa kesi za kufoji vitambulisho ni kwa sababu ya kupigania mali za Chama na kumshukuru rais kwa alichokifanya.

Lengai amesema kwamba akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha alitangaza kiama kwa wezi wa mali za UVCCM Arusha ambapo aanaamini katika wezi hao wapo viongozi wa CCM na Serikali

"Chama cha Mapinduzi ambacho kinajiita chama kikubwa kwa bara la Afrika na kiendelee kuomba omba kwa sababu tu kuna viongozi wameteka nyara mali zake. Rais tunamuheshimu sana kwa juhudi hizo muda unafika itajulikana ipi ngano na yapi magugu na hata sababu za ugomvi na migogoro kwenye UVCCM Arusha uliokuwepo" amesema Lengai

Sabaya ameongeza kwamba siku ya kwanza wakati akiwa anapelekwa mahakamani ni muda mchache aliokuwa ametangaza kiama kwa wezi wa mali za CCM na kuahidi kwamba Kamati iliyoundwa na Rais ikifika Arusha atawapa ushirikiano.

"Leo niseme ukweli Siku ya kwaza nipelekwa mahakamani siku ambayo muda mchache uliopita niliwatamgazia kiama wezi wa mali za UVCCM kwa Mkoa wa Arusha. Nilijua kwamba wapo viongozi wa Serikali na CCM wanahusika kwa kwa kushindwa kuzuia kwa nafasi zao, huo ni uzembe basi itakuwa walihusika moja kwa moja... ghafla nikashangaa ninaitwa kwa kesi za hovyo zisizo na kichwa wala miguu kuhusu vitambulisho. Tatizo halikuwa vitambulisho bali mali za CCM," Lengai
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad