IKIWA ni takribani saa 15 tangu mwanaye ambaye ni Queen wa Filamu za Bongo na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutangaza kuhama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM), mama wa staa huyo, Mariam Sepetu amefungukia kuhusu uamuzi huo wa mwanaye na kusisitiza kwamba yeye bado ni mwanachama wa Chadema.
Mama Wema ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kufuatia kitendo cha Mawanaye kurudi CCM, huku lawama nyingi zikiwa zinamuelekea yeye kama mzazi kwa kutomshauri vema binti yake.
Akiendelea kuzungumzia suala hilo, mama Wema amesema watu wanaomshauri Wema kama wazazi wake si watu wazuri akimtaja Steve Nyerere, huku akisema hawana mapenzi ya kweli na Wema kwani alipopata matatizo walimkimbia, na badala yake CHADEMA ndio waliokuwa wakihangaika naye.
"Nasema haya kuhusiana na Steve, Wema alipopata matatizo hakuweza kutokea central kumuona Wema, leo anashangilia Wema kurudi CCM, lakini akumbuke mimi nitabaki kuwa mzazi, CHADEMA walipoona nataabika nahangaika, waliweza kuja mpaka nyumbani kwangu, kuja kutoa pole, wamemsaidia Wema, napenda kusema CHADEMA ni familia moja, na nilijua kwamba kama kunalolote Wema angerudi kutaka ushauri kwangu, hiki sio kitu chepesi, ni kitu ambacho kimenidhalilisha, kimenitoa utu na najisikia vibaya", amesema mama Wema.
Pamoja na hayo mama Wema amesema Wema atabaki kuwa mtoto wake na hawezi kumchukia kwa sababu ya kuhama chama, ingawa kitendo hiko kimemuumiza.
"Mimi bado nipo chadema sina mpango wa kuhama kwasababu ninahitaji mabadiriko na nitabaki kwenye mabadiriko ya upinzani si vibaya mtoto kuwa CCM mwingine akawa ACT na mama kuwa Chadema na mimi kama mama nitawatambua kuwa ni Watoto wangu" mama Wema.
" Kwa tukio hili lililotokea naweza nikasema amepata ndugu wengine na kuweza kushirikiana ila ukimpata mtu kama steve nyerere ni bomu na mimi nitabaki kuwa mama daima lakini nasema hayo kuhusiana na steve Kipindi wema anapata matatizo hakuweza kutokea hata kuja centrol kumuona wema lakini leo anashangilia wema kutoka chadema kurudi tena CCM lakini kipindi cha matatizo chadema ndio walioangaika na mimi na kuja hadi kwangu chadema kwangu ni familia Bora na nilijua kama kuna lolote wema angerudi kwangu kuomba ushauri