Mambosasa Afunguka Kuhusu Miili Iliyookotwa Coco Beach

Mambosasa Afunguka Kuhusu Miili Iliyookotwa Coco Beach
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kutojitokeza watu kuitambua miili ya wanaume watatu iliyokutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika ufukwe wa Coco kumesababisha uchunguzi kuwa mgumu.

Septemba,2017 wafanyabiashara wa mihogo eneo la ufukwe wa Coco walikuta maiti zikiwa pembezoni mwa bahari zikielea karibu na miti ya mikoko.

Kati ya miili hiyo, miwili ilikuwa imefungwa kwenye viroba na nyingine ikiwa na jiwe lililofungwa kwa kamba.

Kamanda Mambosasa amesema miili hiyo haijulikani ilikotoka na haijatambuliwa kuwa ni ya akina nani.

“Hadi sasa hakuna mtu aliyejitokeza kuja kuitambua ndiyo maana hadi leo hii uchunguzi haujatoa matunda yeyote,” amesema.

Wafanyabiashara eneo la Coco walisema saa nne asubuhi waliona maiti ikielea karibu na mikoko ikiwa imefungwa jiwe kwa kamba na saa nane mchana waliona maiti mbili zikiwa kwenye viroba ndipo walitoa taarifa polisi.

"Polisi walipokuja kuchukua maiti hakuna mtu aliyeruhusiwa kusogelea au kupiga picha. Ulinzi ulikuwa mkali," alisema mfanyabiashara Aziza Ally.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad