Manara Amlilia Mtoto wa 'Mo' Amtumia Salamu za Pole "Tumeumia Sote kwa Msiba Pole sana Kiungo Wetu"

Manara Amlilia Mtoto wa 'Mo' Amtumia Salamu za Pole "Tumeumia Sote kwa Msiba Pole sana Kiungo Wetu"
Kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘MO’ amefiwa na mtoto wake mchanga jana Jumanne katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliandika kwenye ukurasa wake wa Istagram akimtakia pole kwa niaba ya uongozi wa klabu hiyo.

Alisema msiba huo wa mtoto mchanga umewaumiza watu wengi, hivyo akimsihi kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Manara Aliandika hivi kwenye ukurasa wake wa instagram "pole sana kiungo wetu  mnyumbufu @mohammedibrahim04 'Mo' kwa kufiwa na mwanao mpendwa tumeumia sote kwa msiba huu wa mtoto wetu  mdogo kabisa ... kwa niaba ya @Simbasctanzania pokea salamu zetu za pole  kwa msiba huu mzito ww na mama wa mtoto  Inna lilah wainna ilahi Raajiun

Pia mchezaji mwenzake, Deus Kaseke alimtakia pole kwenye mtandao wa huo

TAARIFA: MSIBA WA MTOTO WA MOHAMMED IBRAHIM UPO MBAGALA KIWANGWA

Msiba wa Mtoto wa Mohammed Ibrahim upo nyumbani kwa familia ya Mohammed Ibrahim Mbagara Kiwangwa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad