Mange, Shika, Wema Mtaji wa Watawala -Niki wa Pili

Mange, Shika, Wema Mtaji wa Watawala -Niki wa Pili
Niki wa Pili amefunguka na kusema uwepo wa taarifa nyingi za matukio ya watu maarufu ambazo zinabebwa na kupigiwa makelele kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya jamii ni mtaji mkubwa kwa watawala kuwasaulisha watu juu ya matatizo ya nchi.

Niki wa Pili amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram na kusema kuwa matukio ya Weusi, Wema, Mange Kimambi na kina Dr. Shika ndivyo vitu vinavyowafanya Watanzania kusahau kuhusu matatizo ya ajira nchini, umasikini na ukosefu wa viongozi kwani badala ya wananchi kuanza kuhangaika na matatizo hayo muda wote wanakuwa wakihangaika na matukio ya watu maarufu.

"Sasa hivi ni rahisi kuwasahaulisha watu juu ya ukosefu wa ajira, umaskini, ukosefu wa viongozi nakadhalika, kwa kuwa Media, Social Media kila siku inatupatia utajiri wa taarifa nyingi tukio baada ya tukio. Weusi, Wema, Mange, Dr. Shika, Hamorapa, Meli ya wa china, Trump, Nyimbo mpya, Videos, Karuchi. Utajiri huu wa taarifa na matukio ni jambo jema sana kwa watawala duniani. Na wapigaji wengine ambao ni wananchi tuko bize na taarifa na matukio na bila kujuwa tunakuwa tuna kubaliana na hali ilivyo hakuna pressure wala muda wa kujadili au kupigani ajira, umaskini, Demokrasia, elimu nakadhalika" alindika Niki wa Pili

Mbali na hilo Niki wa Pili amesema kuwa maendeleo ya Teknolojia ni mazuri ila yanaweza kuja kwa njia mbili hasi na chanya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad