Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), DR.Vincent Mashinji amefunguka na kusema kuwa watu ambao ni wezi wa mali za nchi na waliolipelekea nchi hapa ilipofika kwa mambo mabaya ni baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mashinji amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter na kusema kuwa Wazungu hawapaswi kulaumiwa kwani wao walikuja na mapendekezo mbalimbali na viongozi wa CCM ndiyo waliyoyapokea huku akidai chama chake cha CHADEMA kilikuwa kikipinga na wakabezwa.
"Eti Wazungu, wakati wezi ni CCM. Hawa Wazungu wamekuja na mapendekezo CCM ikayapokea kwa mbwembwe na vifijo. Hawakulazimisha, waliridhiana na MaCCM. CHADEMA ikaomba mikataba iletwe bungeni, CCM wakabeza. Mwizi ni nani? Wazungu au CCM? Amkeni Watanzania, adui yupo hapa hapa na si Wazungu" alisisitiza Mashinji
Ni ujinga tu na weak minded African utakaompelekea mtu anaejinasibu kuwa kiongozi katika jamii yetu ya kitanzania kuthubutu kutetea madhambi ya wazungu katika maovu waliotufanyia. Sio wizi wa rasilimali zetu tu ambao wazungu waliuendeleza kwa miaka kwa kupora rasilimali zetu lakini kikubwa zaidi ni uzalilishaji waliokuwawakiutekeleza juu yetu kutokana na imani zao kwamba sisi kama waafrica watu weusi hatukuwa na sifa yakuwa binaadamu wenye haki sawa na wao kwa hivyo hatukustahili kitu chote chote kizuri na cha maana isipokuwa kila kizuri tulipaswa sisi watanzania kama waafrica kukifanyia kazi bure kwa manufaa yao wao . Labda Mashinji kasahau lakini wazungu hawawezi kufanya kosa hilo hasa lile la kuendelea kutupiga kiuchumi na ikiwezekana hata kuwatumia wazawa katika kuendeleza utawala wao kiuchumi kwa mataifa yetu. Kww mfano During German settlement as known for German east Africa, mining took place in all three countries. They were exporting different types of goods such as Gemstones,coffee,rubber and so on to Europe for years. Katika kipindi hicho hakuna cha maana walichokifanya kwa nchi zetu. Sasa kutokezea mtu kuwatetea kwa sababu za kisiasa kwa kweli inasikitisha sana kama watanzania.
ReplyDelete