Aliyekuwa Mbunge wa Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Molel amewataka wananchi wa Siha kutoogopa akisema ametazama mbali hadi kuhama Chama hicho na kudai kuwa hawatajuta.
Akiwa kwenye Kampeni Longido Mollel amesema amehoji kama CHADEMA hawanunui watu huwa wanapeleka wapi Tsh Milioni 360 za ruzuku wanayopata kama chama kwa mwezi.
Mollel amesema kwamba; "Niwaambie watu wangu wa Siha. Msiogope. Mliponichagua kuwa Mbunge nilitakiwa kulitetea taifa na kuitetea Siha. Cheo ni zaidi ya maslahi ya taifa na Siha. Msiogope nimetazama mbali na nimeona mbali hivyo hamtajuta. Nataka kuwamba Rais aliyoko madarakani analitetea taifa".
Godwin Mollel alijivua ubunge Disemba 14 mwaka huu kwa kusema kwamba; “Nimeona nia ya dhati ya Serikali CCM kutetea rasirimali za Taifa, nikaona niweze kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge ili niweze kwenda kujiunga kwa vitendo katika kulinda rasirimali za Taifa letu, aminini watu wangu wa Siha nimeona mbali katika maamuzi haya".
Huna hata Haya. Huku unakokwenda Mali ngapi za umma zimetaifishwa. Sio hao wanaCCM kupitia Ikulu ndio chimbuko la SCROW?
ReplyDeleteArdhi maekari mangapi chini ya awamu ya nne na uongozi wake zimeporwa.?
Ni sahihi ya nani inayotuliza leo Watanzania kuhusu mikataba ya madini, Almasi na dhahabu
kama si viongozi wakuu wa CCM na bado wako huru.?
Ni tembo wangapi wameteketea huku mei zao zikihusishwa na usafirishaji na bado ni viongozi wakuu wa CCM hata hawatachukuliwa hatua yeyote.?
Wauza madawa ni nani?
Waliotaifisha mabenki si ndio hao wakuu wako unaowasikiliza na kamwe hawatafunguliwa
mashtaka yoyote na unawaangalia majukwaani na wameuvaa ukijani na UCCM?
Majmba ya ghorofa ya Kigamboni ni ya nani kama sio CCM?
Ni unafiki wa namna gani. au kutokuwa na akili na utashi.Mtu yeyote mwenye utashi,
Hawezi kurudi na kuunga mkono CCM ambako bado wanalindana na ndiko chimbuko
kuu la kila Tatizo tulilonalo Watanzania.Wengi tumelala, hata kujisomesha wenyewe ili tuamke hatuwezi. Tunabaki kulalama, kuhamahama, bila kuwa na vigezo sababu ujinga umetuzidi.Self education wengi hatuna na wala hatuielewi. Tutabaki kujiyumbisha
na si kuyumbishwa sababu tunachagua ujinga zidi ya elimu ili tujitambue
na kujikomboa wenyewe kiakili.Raisi hawezi kukukomboa kamwe. Na kuwa tegemezi
kwa binadamu moja tu, na kulaza akili zenu ndo maana Tanzania inayumba bila
kujiujua.Kutoka viongozi wa ngazi za juu mpaka chini ni kupwayanga tu. Self
education kujipatia wisdom kabla ya maamuzi ni zero kwa watanzania wengi sana.
Hawana umakini wa kujiinua kintelijinsia , kuhoji, kudadisi, kuweka kumbukumbu
kwa yaliyopita kabla ili tusirudi kule hamna. Watu wanatafuta sifa. Toka
juu mpaka chini, badala ya kuyajua majukumu yao na kuyatekeleza ikiwa ni wajibu
na mujibu wao. Sifa inajitanguliza kama watoto.Na kwa vile hatujielewi,
ni kama yule mzungu mwanamke alisimama na kusema watu wengi hawanaelimu hata
kujua, kuchangia yale ambayo ni mujibu wao. hawaujui hata,ni vigumu sana kulikwamua Taifa
ikiwa asilimia 85 ya watu hawaelewi hata ninalolizungumza. Mtoto ni rahisi kumfundisha
ukimpa maadili. Si rahisi kumfunza mjinga asiyejitambua kuwa yu mjinga.Huyu ni hatari
sana anaweza kuua bila kujijua anamuua Mtu asiye na makosa kutokana na imani potofu.
Tanzania yetu imefikia hapa.Ingawa kunajengeka, ni pesa za watu na nyingi ni za mkopo.
Haina maana ni maendeleo ya nchi. Maendeleo ya kwanza ya nchi yeyote ni elimu mbadala
kwa kila mwananchi kutambua haki,sheria, kushiriki kwenye mipango ya maendeleo na kujipangia mwenyewe na si serikali toka juu. uhuru wa mawazo, kufikiri na kuchangia bila woga hii ni kazi kubwa na tatizo letu kubwa. Imewafanya watu kuabudu miungu watu na kufyata mkia.Haya si maendeleo ya nchi.Watu wote wenye uwezo wa kufikiri mjitafakari kama
mna nia ya kujikomboa na kuleta maendeleo ya kweli na ya kudumu.