Mbunge Mwingine wa Upinzani na Madiwani Wake Saba Kuhamia CCM

Mbunge Mwingine wa Upinzani na Madiwani Wake Saba Wahamia CCM
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri wa Muungano Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kutangaza kuuvuruga upinzani Tanzania kwa kupokea Mbunge mmoja kutoka chama cha upinzani na madiwani wengine saba.


Magufuli amesema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu wa 9 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao umefanyika leo Disemba 18, 2017 mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwepo marais wastaafu.

"Nimepokea majina mengine ya viongozi wa upinzani ambao wanataka kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasaidizi wangu wameniambia yupo Mbunge mmoja anataka kurudi na ameniambia kuwa anataka kuja na madiwani saba kwenye jimbo lake, nasema hiki ni kimbunga na wataisoma namba kweli kweli" alisisitiza Rais Magufuli

Aidha Magufuli amewataka viongozi wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha wanafanya kazi ya kuongeza wanachama wapya katika chama hicho na kuongeza wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa wataendelea kupokea na kuwatangaza watu ambao wanahamia kwenye chama hicho, na kusema kuwa lazima kwanza wajiridhishe ili wasije kupokea na watu wengine ambao hawana mpango mzuri kwa CCM.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umekiri Hadharani na kutumia neno moja nalinukuu kuvuruga. Raisi anavuruga hadharani mchana kweupe. Tutegemee nini Watanzania. Kumbe vurugu imeanzia juu. Na maraisi wote watatu wako kwenye kongomano hili hadharani kuitikia wito wa kuvuruga upinzani. Na Watanzania wanasaliti amri.Hadharani kweupe. Je yanayotendeka gizani si machungu zaidi. Na Watanzania mnayakubali. msilalamike tena.

    ReplyDelete
    Replies
    1. HILO NENO LA KUVURUGA NI LA MWANDISHI, JPM HAJALITAMKA, MSIMLISHE MANENO...mfyuuuuuu

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad