Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema mapema leo asubuhi na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, na waombolezaji wengine wachache wamehudhuria mazishi ya mbwa wa Nassari aliyeuawa na watu wasiojulikana baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na kumpiga risasi.
Mazishi hayo yamefanyika huko huko Arumeru.Mbwa huyo alikuwa ni mlinzi wa Nassari nyumbani kwake ambapo amesikitishwa na kifo cha mnyama huyo aliyekuwa rafiki wake wa karibu.
Mimi sio mtaalamu wa makosa ya jinai lakini hili tukio la kuvamiwa kwa huyu Nassari hakika lina kila dalili yakuwa ni mchezo wa kuigiza au movie alieitengeneza yeye mwenyewe na muhusika mkuu au staring ni yeye mwenyewe. Nassari watu watake kumua kwa tishio gani alinalo kisiasa? Labda majamabazi kutaka kumpora lakini niliangalia maelezo yake binafsi ya Nassari akilalama kana kwamba vyombo vya dola ndivyo vilivyo husika na tukio hilo. Jamani? Vyombo vya dola au serikali ikitaka kumfanyia uhalifu raia haiwezi kumkosa kwani wana watu ambao ni well trained sio rahisi mtu kama Nassari akajibizane risasi na usalama wa taifa au askari polisi alafu Nassari atoke salama hivyo ni vitu vya kuchekesha sana. Kuna sababu nyingi ya Chadema na Nassari kutengeneza hii movie inayoitwa watu wasijulikana. Sababu ya kwanza (1) siasa za matukio...baada ya Chadema na upinzani kukosa hoja za msingi za kushindana na CCM matukio yakuunda na ya kutengeneza ndio imekuwa mtaji wa kutafutia mvuto wa kisiasa kwa wanachama wao na wananchi. Sababu ya pili. Hakuna asiejua yakwamba chama cha Chadema kinakwenda zake kuzimu hilo halina shaka lakini wahusika wanataka kuaminsha ulimwengu yakwamba kufa kwa Chadema ni kutokana na uonevu wa serikali ya chama cha mapinduzi kitu ambacho sio kweli. Sera mbovu za Chadema. Muundo m'bovu wa chama ukanda na umimi ndio halibadri inayoiua Chadema. Sababu ya tatu ni..Siasa za hofu. Hofu ni mmoja ya kati ya mtaji wa maana katika harakati za kumiliki hisia za watu. Wakati mwengine hofu hutumika hata kutawala watu iwe katika mapenzi, ndoa, kazini nakadhalika hofu ni silaha muhimu . Chadema na upizani wanatumia hofu kama mtaji wa kisiasa ili kuvuruga mawazo ya watanzania ili waondowe imani juu ya serikali yao inayowaongoza. Sababu ya nne ya Chadema na upinzani kutengeneza siasa za matukio ni kujaribu kuzishawishi jumuiya za kimataifa baada ya kugonga ukuta hapo mwanzo yakwamba utawala uliokuwepo hivi sasa Tanzania si utawala wa sheria na haki ni wa udikteta, ni njia moja ya Chadema kujitafutia sapota na misaada kutoka mataifa ya nje hata kama ni kuichafua nchi yetu katika jumuiya za kimataifa. Ikumbukwe wazungu Mjerumani,Muengereza na wengineo walizitawala nchi za kiafrica na kuiba kila kitu mpaka watu kwa mamia ya miaka sio miaka mitano 5 au kumi 10 na hakuna waliposhitakiwa some time you can see how stupid as Africans we are in believing white people. Na kwa hili tukio la Nassari kila mtu anajua yakwamba kama uchaguzi utafanyika leo wa ubunge pale katika jimbo lake basi Nassari hawezi kushinda tena hata CCM wakimsimamisha mgombea mpumbavu . Hata matokeo ya chaguzi za madiwani, upinzani hawakuibiwa wala nini wamepigwa haswa kihalali kabisa na hata kama ukirejewa tena hii leo si ajabu Wapizani wakapoteza hata hicho kiti kimoja wichopata. Watanzania wamechoshwa kudanganywa na wapinzani. Wamechoshwa na ahadi hewa za wapinzani na wamebaini ili mabo yao yaende lazima wailete serikali karibu na wanapoishi. Na hawawezi kuileta serikali karibu na wanapoishi kama hayaja wachagua wagombea wa chama tawala. Na kwa bahati nzuri Magufuli anajitahidi kuhakikisha watendaji wake wanakuwa watendaji wa watu hasa wanyonge na kuhakikisha wanawajali. Katika falsa ya utendaji uliotukuka katika kuwahudumia wananchi,watendaji wa serikali siku zote huwa watumwa na wananchi ndio mabosi na serikali ya Magufuli inakaribia utukufu huo kwa hivyo upinzani bado unasafari ndefu kuin'goa CCM na katika kuchanganyikiwa huko kwa upinzani ndiko kunakowapelekea kuzua mambo wengi ya ajabu ili kusavaivu kisiasa.
ReplyDeleteHivi wewe hapo juu, upo unaakili safi. Fanya upelelezi kwanza ndipo uandike hilo. Msicheze na maisha ya watu. Na Waliopigwa mapanga ubasemaje. Kama fikra za wananchi ndio hivi Tanzania bado hatujithamini, wala hatujijui, na ninashangazwa na Mtanzania kuwa na fikra kama hizi. Auea mbwa wake mwenyewe kwa kujitafutia sifa.basi dunia imekwisha.
ReplyDeleteWala usistaajabu, kwa wanasiasa kila kitu kinawezekana, I say never trust them, you better trust a devil than a politician.Hiyo ya kuua mbwa ni trivial.
DeleteWe unashangaa mtu kuua mbwa wake kwa kutafuta kiki mbona hilo ni jambo jepesi hata kama Nassari angejaripua yeye mwenyewe risasi ya paja bado si kigezo cha kuaminisha yakwamba alijeruhiwa na watu wengine kabla ya uchaguzi yakinifu kufanyika. Wakati umefika kwa vyombo vya usalama Tz kuanza kutumia Forensic investigations ili kubain uongo wa kihalifu unaotendwa na watu wenyewe wakisingizia watu wengine.
ReplyDeletehahahaha! Hilo ni picha la kijerumani, unatumia short gun kuua mbwa na maganda yanapotea katika eneo la tukio..DUH Ina maana huyo mpigaji alipomaliza kufanya tukio, akaomba fagio akafagia au akaokota maganda yote 12 ya risasi tehetehe......safari hii sterling atauwawa!!
ReplyDeletealimuua mbwa wake mwenyewe, asitafute mchawi
ReplyDelete