Mke wa Kafulila Kafunguka “Mungu Katunyima Siri Nyingi”

November 30, 2017 Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA Jesca Kishoa ambaye pia ni Mke wa Mbunge wa zamani Kigoma Kusini David Kafulila amekuwepo kwenye headlines kwa zaidi ya wiki moja baada ya Kafulila kuhamia CCM na kumuacha CHADEMA.

Kupitia page yake ya Instagram Jesca ameandika yafuatayo…

UCHAGUZI HUU WA UDIWANI UTOSHE
KUTOA PICHA HALISI YA TAIFA HILI KWA SASA.

Mungu katunyima binadamu kujua siri nyingi za dunia hii ili turudi kwake na kumtambua yeye peke yake kama Mfalme wa ulimwengu.

Ametunyima kuchagua wazazi wa kutuzaa (maana uwenda wengine wangetaka kuzaliwa na watu wa aina ya Trump au Dangote,) ametunyima kuchagua wapi pa kuzaliwa (maana wengine uwenda wangetamani kuzaliwa ulaya na sio Tanzania)

Ametunyima kuchagua malezi ya kulelewa na ndio maana kwa mazingira yoyote watoto wamekuwa wakiishi kutegemeana na mazingira ya wazazi.

Lakini Mungu ametupa nguvu moja kubwa ambayo ikitumika vema huleta matunda mema na majibu ya mambo yote niliotaja juu, Mwenyezi Mungu katika maandiko matakatifu amezitambua Serikali za wanadamu na kupitia hizo endapo kutapatikana viongozi sahihi waliochaguliwa na wengi, ambao kwa uwingi huo ni alama au tafsiri ya chaguo la Mungu, hakika nchi itaneemeka na itatulia.

Ikiwa kinyume chake kwamaana ya alieshinda kuanzia mbinguni sie aliepewa ushindi duniani hakika mambo hugeuka kuwa laana na mateso kwa viumbe wa Mungu, Anguko la Madiwani au Wabunge wanaoshinda chaguzi sio la kwao peke yao na vyama vyao ni anguko la watu wa Mungu waliopaza sauti zao kwa unyenyekevu kupitia sanduku la kura.

WOTE KWA PAMOJA TUKEMEE VIKALI UPINDISHAJI WA MATOKEO BILA KUJALI WEWE NI NANI NA UNA UHUSIANO GANI NA SIASA ZA NCHI ILI KULIOKOA TAIFA HILI.

Roho mtakatifu ana uwezo mkubwa na nafasi kubwa ya kunyoosha mambo sawasawa, ungana na mimi katika maombi maalum juu ya taifa hili usiku huu kabla hujalala popote ulipo – hayo ndio aliyoyaandika Jesca.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtu aliechanganyikiwa au anaelekea kuchanganyikiwa ndie anaweza kuhoji siri juu ya maamuzi ya M/MUNGU. Kwa mtu wa kawaida mwenye kufahamu uwezo wa M/Mungu anaelewa ya kwamba binaadamu hatuachi kujisifia kuwa ni watu makini (smart) pale tunapopata mafinikio lakini hakika mafinikio tunayoyapata ni kwa uwezo wa Mungu. Serikali ya Magufuli isingesimama kama si kwa uwezo na matakwa ya M/Mungu. Licha ya sababu nyingi na visingizio vya hapa na pale kutoka Chadema kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wa madiwani lakini ukweli ni kwamba kuipambanisha CCM YA MAGUFULI na Chadema katika masuala ya uchaguzi kwa sasa ni sawa na kuipambanisha Mtibwa Sugar na Real Madrid. Labda wahusika hawafuatilii maoni ya watu kwenye mitandao ya kijamii. Watu wanaposema chadema wamepoteza mwelekeo hawasemi kwa mzaha bali hio ndio hali halisi. Wakubali wakatae huo ndio ukweli na wasipojipanaga Chadema watateseka sana. Inachekesha sana unaposikia Chadema wana mikakati ya kupambana na serikali kinguvu? Magufuli na serikali yake wanavyombo vya ulinzi na usalama lakini kubwa kuliko yote Magufuli na serikali yake sasa wanasapota kubwa ya ndani na noe Tanzania kulinganisha na tawala zilizopita. Na Watu wanaposema Zito Kabwe ana matatizo ya kujiona kuwa ni mwanasiasa wa ulimwengu mwengine na watu wengine wote ni wajinga wakati kiuhalisia Zito wa sasa huwezi kumlinganisha hata na robo ya ubora wa Joseph Msukuma sasa hapo wapinzani kitu gani kinachowapelekea kujinasibu kuwa na uwezo kuin'goa CCM madarakani? Waswahili wanasema wengi wape usipowapa watakunyang'anya.

    ReplyDelete
  2. Nakupinga kwa nguvu zote wewe hapo juu. Ni wachache sana Tanzania wenye busara, kuelewa kwa mambo kwa hali ya juu. Nimemsikiliza pia Mke wa Kafulila, Sijui Kafulila alikwenda hija gani. Na kwa wakati wote huo ni mke wake tu na si CCM. aliyempa kiwewe Kafulila ni wizi wa mali za umma kupitia CCM. Ni uongo wa viongozi wa juu wa CCM. Ni taifa gani linashindwa kukomesha rushwa. Ni taifa gani uongozi umekidhi uongo na kutokumjua ni nani aliyeingiza magari. Ni taifa gani watu wakimhisia mtu aliyeleta magari badala ya kufanya uchunguzi na upelelezi Raisi anakuja juu na kuwatishia watu hadharani mahakama na polisi wa kuchubguza mambo yeye anawakataza watu kutoa hisia wanazozijua. Sasa kama Watanzania na Wanaccm tunaaakili safi, mtu mmoja hawezi kutumbua kila kitu bila msaada wa wananchi. Mnakubalije kufungwa wote midomo na kumruhusu mtu mmoja awadictate kama wote ni malimbwende., kama si ujinga ni nini? Hata katika nyumba zenye ustaarabu watoto wanauhuru wa kuchangia. ukiruhusu kuna amani , upendo, mafanikio na maendeleo kifamilia.Najiulza , hivi Watanzania hatujitambui.
    najiuliza, Kibiti, watoto wote wamepoteaje tuna ulinzi, na serikali. leo inakurupuka. kufukuzJe ndo hawa wanaelea baharini? wote hao, tuna mapolisi kibao. Hivi kweli mioyo ya viongozi tuliowakabidhi madaraka inalalaje usiku wakijua Wananchi wanapotea, wanauawa, wanatekwa na mnawaaminije na hizo kazi? Cha kushangaza, Wengi Watanzania bado wanafurahia huu utawala hivi hamjaguswa kwa namna fulani na kaka, dada, shangazi, mjomba, binamu, mkeo, mume, mtoto, rafiki, au jirani aliyeyedhurumiwa, pigwa, uawa, potea,nyanganywa ardhi, bomolewa nyumba, kafia wakati wa kuzaa. Mnashindwa kupaza sauti sababu ya uoga. kukosa ajira. wengi wasomi wanapapatika kwa Msukuma na mabilioni. Kisa pesa ajira, watu wanapoteza utu kujipendekeza kuajiliwa kushuka kihadhi ni wasomi waliobobea hata nje, wameshindwa kujiajili, wanajiuza. Ni aibu gani?
    chonishangaza zaidi, kumwacha Lisu nyinyi mnaohama, kupatwa na majanga mazito akipigania na kudai haki za Watanzania. Wanamtelekeza, kufuata CCM. mkipatwa na majanga mtakwenda wapi. Mtajiuza. E binadamu, Mke Kafulila kasema tunahitaji kumjua Mungu, kuomba vipaji vya roho Mtakatifu, kujitambua, kuchajiwa kiakili, kuabudu na kusali , kupata hekima ya kujitambua, kujiheshimu, kushauri, na kupokea ushauri. Wengi wenye akili za kufikiri chache hawawezi kuelewa undani wa hili. Hawana uwezo. Nilimfuatilia yule mzungu mwanamke aliongea kiswahili safi sana. Aliuliza kama elimu yako ya kufikiri ni ndogo sana utawezaje kuchangia iwapo huelewi, na Serikali haina hata mpango wa kutoa elimu hiyo, ikijua watu wakiamka ni wao kisheria watawekwa ndani. Na kuna dalili ya kila kitu, viongozi wetu wa juu wengi tukiwa na katiba mpya na huru wengi ndani.Na matumbo joto. Lakini Watanzania wengi ingawa wanajua ukweli ni ndumila kuwili. Si wazalendo. Wapo radhi kujipatia leo na kutokujali watoto wao kesho na vijukuu. Bado wanafikiri kule kupeana kutaendelea, kufichiana ukweli, kubebana. Akipata kashiba leo kasahau. Ndio Watanzania wendi dhidi ya usomi wao ndo wako hivi. Pia Watanzania tunaudhaifu tofauti kikabila. Kunamakabila wanajituma sana , kielimu na kiutendaji pia. Kunamakabila uduni wa elimu na hawajitumi. Lakini wote tunataka tuwe sawa kipesa na kimaendeleo. Ndo maana wengi wasiokuwa na nidhamu za jadi kujituma, kujiendeleza kimasomo, hata ukimpa cheo si rahisi kujibadili kimaisha sababu kazubgukwa na watu wa hali ileile.Na inakuwa ni mzigo mkubwa sana. Kukomesa haya kunahitaji kiongozi wa namna ya pekee sana, Achague viongozi pia wenye mienendo ya utambuzi wa hali ya juu. Na ni wachache sana. Wengi wamesoma lakini hawana hili ninalolizungumzia. Wengi hawajasoma lakini wanautambuzi wa hali za juu. Degree za mashuleni si kipimo. Lakini sisemei mtu kama Makonda. Makonda kabebwa na anamiminiwa sifa, misaada ambayo haijengi uchumi wala fikra za Watanzania kuwanasua kielimu. Badala yake nyuma ya pazia ya hii misaada inaua maendeleo na inajenga tegemezi na pia inkuwa kama hongo kutoka kwenye mataifa haya kunyima zaidi uhur wa Mtanzania.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad