Mkuu wa Mkoa Aitaka Takururu Ichunguze Ofisi yake

Serikali Mkoani Mara imeiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi wa upotevu wa fedha zaidi ya Tsh 3.5bn katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na miradi ya maji mkoani humo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima katika kikao cha pamoja cha watendaji wa TAKUKURU, Mahakama na Jeshi la Polisi. Kikao hicho kiliitishwa kwa malengo ya ofisi hizo kujitathimini katika utendaji kazi.

Malima ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huo mwishoni mwa mwezi wa Oktoba amesema katika ofisi yake pekee, amebaini ubadhirifu wa zaidi ya Shilingi milioni 500.

“Kwenye miradi ya maji ya mkoa huo, kuna zaidi ya Shilingi bilioni tatu hazionekani. Kila ninapokwenda katika mkoa wa Mara, kila ninapokanyaga watu wanalia na shida ya maji. Tena ni aibu zaidi kwetu hapa maana tupo hapa na ziwa lipo lakini watu hawana maji. Hatuwezi kuvumilia haya, lazima hatua kali zichukuliwe,” amesema Malima.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi hamjielewi bado. Mtu atajichunguzaje mwenyewe. Tukukuru ni kitengo cha cCM. mmeshaona Wanaccm wanafungwa kwa jambo lolote. Ukitaka kinga ya mauaji, wizi, ufisadi, uporoji, jiunge na CCM. Watawafunikeni macho watabakiana kila walichokiiba. Na bado watateuliwa kulindana tena, na tena na tena. Ukiingia CCM upo kwa Mungu. Hawa ni miungu watu. Hakuna kitu. Umeshuhudia mambo ya Lisu, maiti isiyotambulika. Ni Watanzania wenetu. Ni watu wasiojulikana kwenye mfumo mpya unaotumika na chama tawala kwa sasa. Inawataka Watanzania wote warudi CCM. ni mbinu yao ya kwanza, Hata waliopigwa, fungwa kwa kuonewa, wengine ndugu zao na marafiki zao wamepoteza maisha, au kutoweka bila kujulikana. Waliibiwa na kunyanganywa raslimali, bomolewa majumba kwa visa, lakini cha kushangaza, CCM imefanikiwa na inazidi kuendelea kuwarudisha hawa wote tena CCM.Huoni kitendawili hiki. Uliodhania mashujaa, wenye elimu, uvumilivu, hekima wamesalimu amri kwa CCM. kwa mtu mmoja Magufuli. Dhambi kubwa. Kama mungu yupo . Sidhani kama kuna Mungu. Kuna Mungu pekee wa CCM tu. Ni Mungu wa Magufuli na CCM na viongozi wote wa CCM. AAbudiwe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad