February mwaka jana wakati AY akitambulisha remix ya ngoma yake ya Zigo ambayo amemshirikisha Diamond jina la Motra The Future liliibuka katika interview iliyofanyika XXL ya Clouds Fm.
Aliyeibua jina la Motra The Future ni Diamond wakati akitaja baadhi ya wasanii wa hip hop ambao bado hajafanya nao kazi, wasanii waliotajwa ni Motra na Fid Q.
Uzuri ni mwamba mwaka mmoja mbele muimbaji huyo wa WCB aliweza kushirikishwa na Fid Q katika remix ya ngoma Fresh, hivyo wakawa wamemalizana.
Karibu Motra
Motra The Future ni moja mmoja wa marapper ambao muziki wao unawakilisha kule wanapotokea, ana ubabe wake linapokuja suala la free style.
Moja ya ngoma zake zilizofanya vizuri ni pamoja na One Day aliyofanya na Ruby, Sina Koloni aliyofanya na G Nako, Baddest akishiRIkiana na Bullranking, Uswazi na nyinginezo kibao. Hata hivyo amekuwa na uwezo mkubwa wa kurudia/kufanya cover za ngoma za wasanii wengine na kuzitendea haki.
Ameweza kurudia ngoma ya Madee ‘Yote Maisha’ ambayo alimshirikisha P Funk Majani, hata hivyo katika kurudia ngoma hiyo aliyopita na verse zake alimshirikisha Banana Zorro.
Hiyo ilikuwa ni baada ya kufanya hivyo katika ngoma ya Mwana FA inayokwenda kwa jina la Asante kwa Kuja ila yeye akaipa jina la Mbishe Gani, pia alifanya hivyo katika ngoma ya Bill Nass ‘Chafu Pozi’ na kuipa jina la Hakuna Chafu Pozi.
Sasa baada hizo hatimaye amerudia ngoma ya yule msanii (Diamond) aliyesema anatamani kufanya kolabo. Hapo jana aliachia remix ya ngoma ‘Waka’ ya Diamond aliyomshirikisha rapper Rich Ross kutoka Marekani.
Remix hiyo inakuja ikiwa ni wiki moja tangu ngoma hiyo kuachiwa official, hata hivyo bado wawajaingia studio kufanya kazi yao ya pamoja kama ilivyonukuliwa hapo awali.