Msanii wa muziki wa bongo ambaye ni miongoni mwa wasanii wachache walioanza na game ya bongo Fleva, Paul Mbena maarufu kama Mr. Paul, ameweka wazi sababu iliyomfanya yeye aache muziki.
Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live, Mr. Paul amesema kipindi ambacho wao walikuwa wanafanya muziki kulikuwa na changamoto nyingi ambazo alishindwa kuhimili, na kuamua kukaa pembeni kwa muda kufanya mengine.
“Kipindi ambacho sisi tunaanza muziki soko halikuwa kama sasa hivi, kuliwa na frustration nyingi, nikaachana nao kwanza nikarudi shule nikapiga degree kisha masters nikaingia ofisini, lakini sasa hivi naona vitu vimebadilika, watu wengi wana smart phones wanadownload nyimbo ikitoka tu, naona vijana wana chance kubwa ya soko”, amesema Mr. Paul
Mr. Paul ameendelea kwa kusema kwamba sasa hivi ana mpango wa kurudi kwenye game ya bongo fleva, na yuko tayari kushirikiana na wasanii wa sasa ili kupata kazi zenye ubora zaidi.
“Kama kuna uwezekano wa kuandikiwa muziki, nitawaacha waniandikie kama kuna masuala ya kulipa pesa nitalipa waniandikie ili niweze kwenda nao sawa”, amesema Mr. Paul