Mrema Amvulia Kofia Rais Magufuli
3
December 09, 2017
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amepongeza uamuzi wa Rais John Magufuli wa kutoa msamaha kwa wafungwa na kumuelezea kama Rais mwenye upendo wa aina yake.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi, Mrema amesema ni wazi kuwa Rais amesikia kilio cha watu na kuamua kufanya ubinadamu ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.
“Namvulia kofia kabisa, huyu ni Rais msikivu, ana mapenzi ya kweli kwa Watanzania naweza kusema tumepata mtu ambaye tulikuwa tunamtaka,”
Mrema amesema upo uwezekano kuwa Rais alikuwa hapewi taarifa sahihi kuhusu hali ya magereza.
“Magerezani kuna uozo, wapo watu wengine wanajaa kule kwa makosa ambayo wanaweza kulipa faini tu wakatoka,”
“Nilianzisha kampeni ya kuwalipia faini wafungwa ambao walishindwa kujilipia lakini kutokana na maslahi ya baadhi ya watu nikaambiwa nisitishe kwa madai kuwa wafungwa hao hawajajutia makosa. Hii si sawa, naomba watu wa magereza wabadilike hakuna sababu ya kuwajaza wafungwa kule ambao wanatakiwa kutoka,”
Tags
Mrema Nakubaliana na wewe Mia kwa Mia... Huyu si Raisi wa Rakhisi... Huyu Game changer si Bullzoder wa D6... Huyu ni Msikivu na anachukua Uamuzi Stahiki inapohitajika bila kupoteza wakati.
ReplyDeletena Mimi nasema kuwambia waachiwa kuwa Baba yetu huyu ana Imani juu Yao na amewahurumia wao na Familia zinazo wazunguka na amesikia kilio chao kama sisi tunavyo lia na Ardhi zetu za Winde...B'gmoyo.
Magu Baba..!!!
Mungu akuwe na akulinde.
Mlio achiwa tunakuombeni chonde chonde Msimwangushe Raisi wetu na Imani yakw Juu yenu.
Rudini Uraiani na muwe Wazalendo na Raia wema. Nchi yetu ni Salama na tunahitaji Amani yenu Uraiani kwetu.
Karibuni sana muungane na Familia zenu na kuwaondolea dhiki za kowakosa kwa muda wote mliokuwa hamko nao.
Iwe ni Furaha na Amani kwenu.
karibuni na tujenge Taifa kwa pamoja.
Na tufanye kazi kwa bidii kweli kwelinchi inakuhitajini katika uzalishaji na kulitumikia Taifa. kumbukeni hii ni awamu ya
HAPA KAZI TU NA SI VINGINEVYO.
ASANTE BABA JPJM. Watakuelewa tu.
Re: Mr Mrema km ipo kt uwezo wako, tafadhali msaidie huyo aljyenusurika kunyongwa mwenye umri wa miaka 85. Atakuwa mgeni wa nani? Alikaa jela toka Labda 1972. Tz imebadilika sana Labda atapotea asijue pa kwenda, umri umekwenda na pengine nguvu zimepungua pia, na mwenzi wake pengine, km alikuwa naye , ametangulia. Makazi nina mashaka km bado yapo. Akienda jela hata bababara ya nelson Mandela tu ilikuwa bado haijajengwa. Tafadhali msaidie
ReplyDelete1972 usafiri ulikuwa DMT, UDA ilikuwa bado. Mabasi ya mikoani ni Teeteeko. Airport transfers ni ile ndogo ya sasa ilikuwa bado. Magazeti-uhuru. Mzalendo na daily news. Population watu millions 12 Dar haikuwa na msongamano. Chama cha siasa TANU na AFRO wakati mfumo ni ujamaa na kujitegemea chini ya Mwalimu Nyerere. Agizo la makao makuu dodoma lilikuwa bado. Burudani izoziacha is nyingi haiko. Dar jazz, AFRO 70 and na Balisidya, safari trippers and marijani, safari nkoye, tabora jazz, Morogoro Jazz na mbaraka mwinshehe, Juma kilaza, shakila na Juma balo. Km alizoea kuona Frelimo wakipitapita basi hawapo wamerudi kwao kufuatia uhuru wao mwaka 1975 na Samora alikuja kuwa rais, Lakini kwa sasa Marehemu. Kaburu A. Kusini, Rhodesia na Namibia alishafungasha na Mandela alifunguliwa na sasa ni marehemu. Sasa hivi tuna TV na communication ni Simu. Kigamboni unaweza tu kutembea. Maradhi yalizuka km ukimwi na taadhari in Atakuwa. Vyama vya siasa pia ni vingi na ujamaa ni kama uliondoka kinyemela bila hata kutangaziwa officially.
Delete